VIJANA 400 WAJIHUSISHA NA VITENDO VIOVU KAHAMA
Meneja mkuu wa kampuni ya Acacia Michelle Ash akikabidhi vifaa mbalimbali vya kufania usafi wa mazingira kwa mmoja wa vikundi vilivyosaidiwa na mgodi huo mbele ya kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Zabron Donge.Wananchi wa Kata ya Bugarama wakishuhudia jinsi mgodi unavyo gawa msaada huo kwa vikundi vya vijana wanaoishi mazingira magumu ambao wanajihusisha na vitendo viovu vya uvutaji bangi na madawa ya kulevya.
Meneja mkuu wa kampuni ya Acacia Michelle Ash akimkabidhi afisa tarafa wa kahama mjini Julius Chagama aliyemwakilisha mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya.
Badhi ya vijana wanaoishi katika mazingira magumu wanaojihusisha na vitendo viovu waliojiunga katika vikundi ili kusaidiwa na mgodi huo
Baiskeli zilizotolewa siku hiyo na mgodi
Meneja mkuu Michelle Ash akiwahutubia wananchi
ZAIDI ya vijana 400 wanaoishi vijiji jirani na mgodi wa dhahabu Bulyanhulu katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama wanao jihusisha na vitendo viovu ya uvutaji bangi na madawa ya kulevya wamepatiwa msaada wa vitu mbali mbali vya kufanyia usafi wa mazingira vilivyoghalimu zaidi ya shilingi milioni 16.5 ikiwa ni moja ya kujiajili wenyewe.
Akikabidhi msaada huo meneja mkuu wa kampuni ya Acacia Michelle Ash alisema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuwasaidi vijana hao waweze kujiajiri wenyewe ili kuondoa mawazo mabovu ambayo na kuepuka kujiingiza katika makundi mabaya na vifaa hivyo vitawasaidia kujipatia fedha halalali kwa kufanya usafi wa mazingira.
Alisema licha ya mgodi huo kudumisha mahusiano kwa jamii na majirani zake mgodi umeamua kuwasaidia vijana hao kwakuwa wamejitambua kuwa nao ni sehemu ya jamii na kuamua kuunda vikundi na kusema hawatarudia kufanya matendo maovu kwa jamii na vifaa hivyo watavitumia kuboresha mazingira katika maeneo ya vijiji hivyo.
aidha meneja huyo alisema vifaa hivyo ni pamoja na matoroli baiskeli 19 na vitu vingine vilivyo ghalimu kias cha shilingi 19,500,000/= huku akisema lengo la mgodi ni vijana hao pia wasiwe tegemezi kwa jamii pia waweze kuibua fursa ya kujiwezesha wenyewe.
Kwa upande wake mwenyekiti wa ushirika wa vijana Mohamed Abdul alisema isingekuwa mgodi huo kuwezesha vijana walikuwa hatarini kuwa mazezeta na vibaka waliokithili na baadhi yao wangeweza kupoteza maisha hivyo aliushukuru mgodi kwa kuwashauri kuunda vikundi ili wasaidiwe.
Abdul alisema kuwa kwa sasa kikundi hicho kina vijana 400 ambao hadi sasa wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na masuala ya kukaba na kupora pesa kwa wananchi hasa kutokana na mgodi kuwaahidi kuendelea kuwasaidia.
.
“Wakati mgodi haujaamua kutusaidia, sisi ni watoto yatima na tunaishi mazingira magumu hatuna wazazi katika vikundi hivi wengi wetu tulikuwa tunajihusisha na vikundi viovu vya uvutaji bangi hivyo mimi kama mwenyekiti wa kikundi hiki nitahakikisha vifaa hivi vinatusaidia katika kutunza mazingira,pia huu ndiyo mtaji wetu,’’alisema Abdul na kuongeza.
Naye afisa tarafa kata ya Kahama mjini Julias Chagama akimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya alisema kuwa serikali inatambua kuwa mgodi unatekeleza majukumu yake na kufanya baazi ya kazi zilizotakiwa kufanywa naserikali za kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hivyo kuwataka wananchi hao kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wanaofanya maendeleo.
Pamoja na hilo kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Zabron Donge aliwataka vijana hao kutunza vifaa walivyo walivyopatiwa na wawekezaji hao na kusema halmashauri ya msalala itaangalia uwezekano wa kushirikiana nao ili kuzidi kuwasaidia.
Habari na Paul Kayanda
0 comments:
Post a Comment