Tuesday, September 16, 2014

MAHAFARI YA KWANZA YA DARASA LA SABA SUNSET ENGLISHI MEDIUM INAYOPATIKANA KAHAMA

MAHAFARI YA KWANZA YA DARASA LA SABA SUNSET ENGLISHI MEDIUM INAYOPATIKANA KAHAMA 


 CAPTAIN Omary Hanzuruni akiwaongoza mgeni rasmi katika mahafari hayo,Zacharia Misana Afisa uhamiaji Wilayani Kahama pamoja na Mkurugenzi wa mji  wa Kahama, Felix Kimaryo kwenda kukagua gwalide la vijana kutoka shule ya msingi Sunset
 Mlezi wa shule ya Sunset, Mahamoud Jaha kulia akiwa sambamba na Afisa uhamiaji ,Zacharia Misana wakiongozwa na captain Hanzuruni kuelekea jukwaa la vijana machachari katika kuhakikisha wanamazoezi mazuri ya kulinda Taifa
                Vijana wa kikosi kutoka Shule ya Sunset wakiwa wamejipanga kikakamavu
 Viongozi hao wakisindikizwa na mlezi wa Shule hiyo wakiwakagua maaskari hao kuona shughuli za kiusalama zinatimizwa vizuri
 Captain Hanzurini akiwatambulisha maaskari wake kwa wakaguzi wa  vikosi hivyo
                                                      Twendeni na huku muone
 Afisa huyo wa Uhamiaji mwenyesuti ya kaki pamoja na mlezi wa shule hiyo wakiwa wamesimama kikakamavu huku wakiangalia kama maaskari hao wako sawa
                                         Hili ni jeshi la JKT likiwa tayari kwa lolote
                        Wakiangalia jeshi la Magereza  mchanganyiko na la Uhamiaji kwa makini
                                                     Simama imara
                                               Katiza uone cha moto
                                   Captain Hanzuruni akiwa mbele ya maaskari wake
                                                              TUPO IMARA
                                           Jeshi la majini likionyesha umahili wake kazini
                                                                     Waogope hao

                                                     Wakiwa tayari  kukabiliana na maadui
                 Wakipita huku  macho nyuma nakusonga mbele bila kupindisha mistari
                                             Wakiwa katika mwendo wa haraka
                                                 Walimu wakiwa pamoja na wanafunzi wao
 Mlezi wa Shule ya Sunset Mahamoud Jaha mweye suti ya blauni akiw na skafu shingoni kushoto kwake ni Afisa Uhamiaji akiwa wa Wilaya ya Kahama, Zacharia Misana, mwenyekaundasuti ni Mkurugenzi wa mji wa Kahama,Felix kimaryo  wakiwa meza kuuu  wakiwatazama wanafunzi wa shule hiyo wakati wakionyesha maonyesho ya jeshi la ulinzi yaliyoandaliwa na shule hiyo.
                     Baadhi ya walimu kutoka shule mbalimbali za watu binafsi wilayani humo
                                                       WAKILITAWALA JUKWAA


                                              Bendera za Tai
                                                 Wapiga bendi la gwalide mahili wa shule hiyo
                                                        Jinsi palivyokuwa
                        Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa katika picha na kwenye mahafali hayo
                                                    TUMEPENDEZA
                                                               USITUSOGELEE

                                                         TUNAPIGA PICHA
                   TUMEMALIZA DARASA LA SABA TUKIW NA AFYA NZURI TUMEFURAHI
                          UKITUONA TUPO KAZINI PIT MBALI CHEZEA SIRAHA WEWE
 Maaskari hawa wamepata nafasi ya kuzungumza na blog hiii na kusema kuwa hata wakifanikiwa kuingia katika kidato cha sita hapo baadye mungu akipenda watajiunga na jeshi la kulinda Taifa JKT na kuahidi kulitumikia taifa hili vyema.
 Hiki ni kikosi cha makomando wa Tanzania wakionyesha umahili wao wa kung'fuu mbele ya viongozi wao pamoja na mgeni rasmi
                                         Komando akimkabili adui
                                                     kikundi cha kwaya cha shule hiyo
 Wanakwaya wakiwa wamependeza huku wakiimba kwa kuringa na kujidai kwa nyimbo yao nzuri
 Kikundi cha ngoma asili kilichoandaliwa na meneja wa shule ya msingi Sunset,Nadine Mahamoud
 Tunajivunia  kusoma katika shule nzuri yenye walimu waliobobea kwa masomo ya kiingereza pamoja na Computer
 Kikundi cha makabila ya wahaya kwa kina pacha wa Saida kalolo kilichoratibiwa na Meneja huyo Sunset kilisisimua watu waliohudhulia mahafari hayo hali iliyowalazimu makabila mbalimbali kwenda kucheza na kulishambulia jukwaa hilo

 Kikundi cha wahaya kilichoibua hisia za mamia ya watu waliohudhulia mahafari hayo kililitawala jukwaa hilo



wananchi wengi kanda ya ziwa hawathamini elimu

IMEELEZWA kuwa kitendo cha Wananchi wengi waliopo katika kanda ya ziwa kutokuthamini Elimu kwa kiasi kikubwa kimesababisha baadhi ya fursa nyingi zilizopo katika kanda hiyo hasa katika Migodi huchukuliwa na watu kutoka katika mikoa mingine iliyopo nje na migodi hiyo.
Hayo yalisemwa juzi na Afisa wa uhamiaji wa Wilaya ya Kahama  Mkoani Shinyanga,Zacharia Missana katika Mahafali ya kwanza ya shule ya msingi Sunset yalifanyika mjini Kahama na kuongeza kuwa kwa sasa watu wa maeneo hayo lazima wabadilike.
Missana alisema  kuwa katika Dunia ya sasa huwezi kupata hata fursa ya kufanya kazi katika Migodi iliyopo katika Wilaya ya Kahama bila ya kuwa na Elimu ya kutosha hali ambayo kwa wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika juu ya kukosa fursa za kupata kazi katika maeneo hayo ya migodi nakwamba wanatakiwa  kujua elimu ndio kipaumbele.
Afisa Uhamiaji huyo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya katika Mahafali hayo alisema kuwa kwa sasa wanachi wa maeneo hayo hawana budi kushirikiana na wawekezaji waliopo katika Wilaya ya Kahama katika masuala mazima yanayohusu Elimu ili iwe rahisi katika kufanikisha uhamasishaji wa elimu.
Aliwataka Wakazi wa Kahama kuamka katika suala zima la Elimu na kuongeza kuwa hata mauwaji ya vikongwe yalioshamiri katika maeneo ya wilaya ya Kahama na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla yanaweza kuisha kama kila mtu atakuwa na Elimu ya kutosha na kuwa msaada mkubwa kwa wengine.
Kwa upande wake Mlezi wa Shule ya Sunset Mahamoudu Jaha alisema kuwa suala la Elimu katika dunia ya sasa sio la kubeza na kuishauri serikali kuzidi kuboresha miundo mbinu kwa kiasi kikubwa suala la elimu ili kila Mtanzania aweze kusoma na kusomesha watoto bila ya kuwa na malalamiko yeyote.
Nae Mkuu wa Shule hiyo Eliasafu Bayaga katika  risala yake aliyoisoma mbele ya mgeni rasmi katika mahafari hayo alisema  kuwa shule hiyo ilianza mwaka 2010 na kuwashauri wazazi kuwatunza wanafunzi majumbani kwao kwa nidhamu wakati wakisubiri matokeo yao hali ambayo itawafanya kuingia kidato cha kwanza wakiwa katika maadili mema.
Shule ya Sunset iliyopo mjini Kahama jumla ya Wanafunzi 23 walihitimu darasa la saba huku wanafunzi 13 wa shule ya awali wakifanikiwa kupata vyeti vya kujiunga na darasa la kwanza kwa mwaka ujao katika shule hiyo.
PAUL KAYANDA-KAHAMA SHINYANGA,


My Blogger Tricks
blogger

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.