Wanafunzi watakiwa kusoma wakiwa na ndoto za maisha
Haya ndiyo mazingira ya shule ya msingi Rocken Hill Academy ya mjini Kahama
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akitoa ufafanuzi juu ya usalama wa raia wema na mali zao wakati akizungumza na wazazi na walezi wa watoto waliohitimu elimu ya msingi katika shule ya msingi Rocken Hill Academy iliyopo mjini Kahama mkoani Shinyanga katika mahafari yao.
Alexander akiwaasa watoto waliohitimu masomo yao ya elimu ya msingi
Mkurugenzi wa Shule hiyo,Alexander Kazimili akitoa nasaha zake kwa watoto pamoja na wazazi na walezi wa watoto hao.
Wahereheshaji kutoka vikundi vya sanaa nao wakitoa shoo mbele ya wazazi wa watoto hao
Mkurugenzi wa shule ya msingi Rocken Hill Alexander Kazimil hapo akicheza pamoja na wanafunzi siku ya Mahafari yao waliohitimu elimu ya msingi sambamba na wazazi na walezi wa watoto hao.
Justus kamugisha kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga
WANAFUNZI wanaomaliza darasa la saba
hapa nchini wametakiwa kusoma kwa bidii katika Elimu ya juu huku wakiwa na
ndoto za maisha yao hapo baadaye hali itakayoweza kuwasaidia pindi wanapoanza
maisha ya kujitegemea bila kusubili msaada wa wazazi wao.
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi wa
Shule ya Rocken Hill Alexander Kazimiri wakati akizungumza katika mahafali ya
11 ya shule hiyo tangu kuanza kuhitimu kwa Elimu ya msingi katika shule hiyo na
kuongeza kuwa kusoma bila ya kuwa na ndoto za baadaye haisaidii chochote
katika maisha .
Kazimiri alisema kuwa kazi ya kusoma
ni pale unapokuwa na maono ya baadaye ya maisha ikiwa ni sambamba na kusimamia
nidhamu unapokuwa shuleni na kusikiliza mafunzo kutoka kwa Walimu
hali ambayo inaweza kuleta mafanikio makubwa katika maisha.
“Wazazi kazaneni kusomesha
watoto wenu kwani elimu ya watoto wenu ni Bima ya uzeeni itakayowasaidia
kuwatunza ninyi hivyo endeleeni kuwekeza katika suala la elimu katika kipindi
hiki cha mapinduzi ya Sayansi na Teknolojia pia kama unataka kuwa Mhandisi
lazima upende kusoma masomo ya Sayansi kama vile Phizikia, Bailogia pamoja na
Kemia hali ambayo inaweza kukusaidia katika kufikia lengo la maisha yako ya
baadaye”, Alisema Alexander Kazimiri Mkurugenzi wa Shule ya Rocken Hill
Academy.
Mkurugenzi huyo aliwataka Wazazi wa
watoto wanaohitimu Elimu hiyo ya Msingi kujua kuwa Wanafunzi ndio bima yao ya
uzeeni na kupitia kwao wanaweza kuona matunda yake pindi wanapofanya vizuri
katika masomo yao hali ambayo wanaweza kuona mafanikio pindi wanapopata kazi
nzuri na kuweza kuwasadia.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo
yaliojumuisha jumla ya Wanafunzi 220 alisema kuwa
Kwa sasa katika nchi ya
Tanzania siasa zake zinahitaji usomi wa hali ya juu na kuongeza kuwa siasa za
sasa sio kama zile za siku za nyuma.
Kamugisha alisema kuwa Siasa za sasa
sio za kuvamia tuu kama ilivyokuwa hapo awali bali kwa sasa huna budi kusomea
na kuongeza kuwa hata katika vyuo vikuu hapa nchini kwa sasa kuna watu
wanaosomea Elimu ya Siasa hadi kupata Stashahada au Shahada kwa ajili ya Elimu
hiyo hiyo.
Pia Kamanda Kamugisha alisisitiza
masuala ya Ulinzi na amani nchini na kuwataka Watanzania kuacha kuwahifadhi
Wageni wanakuja katika nchi yetu ambao hatuwajui kwani kwa sasa wema wa
Watanzania umepita uwezo wa kuwakarimu hadi Wageni ambao hata hatuwajui
wapotoka.
“Sisi tumekuwa tukiwahifadhi wageni
kwa kiwango cha juu lakini kama na sisi tukienda katika nchi zao ukarimu huo
haupo kwani wenzetu wamekuwa wakijenga hofu kubwa kwa wageni tofauti na ukarimu
tunaowafanyia Watanzania wanapokuja hapa nchini”. Alisema Kamanda Kamugisha.
Hata hivyo Kamanda huyo alisisiza
Wazazi kuwapeleka Watoto wao Shule ili kuepuka majanga yanayotokana na ukosefu
wa Elimu kwani hata mauwaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanakuwa yakitokea
mara kwa mara yamekuwa yakitokea kutoakana na watu kutokuwa na elimu na
kuongeza kuwa kama watoto watasomeshwa na kuelimika hali itakoma.
Habari na Paul Kayanda-Kahama
0 comments:
Post a Comment