Monday, June 9, 2014

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE WAWILI KUNUSURIKA NA KIFO MACHIMBONI MWIME KAHAMA

 Waandishi wa Habari Appolinary wa Radio Kahama fm Na Neema Sawaka (Jambo leo ) wakiwa wanaandika majina ya watoto waliopo katika machimbo ya Mwime Kahama
                 Wachimbaji wadogo wa Machimbo ya Mwime wakiwa katika picha ya Pamoja

                       Hawa wanaoonekana pichani ni Baadhi ya wachimbaji wadogo  ya Mwime


                                                      Picha ya  Marehemu Ezekiel Moshi  zizi
 Wachimbaji wakiwa wameuzunguka mwili wa Marehemu katika Banda lililopo katika Machimbo hayo
            Mwandishi wa Redio Kahama fm akiwa katika harakati ya kutimiza majukumu yake
 Gari la Jeshi la Polisi Willayani kahama likiwa tayari kutoa msaada wa kuupeleka mwili wa marehemu Ezekieli  katika chumba cha kuhifadhia Maiti Katika Hospital ya Wilaya ya Kahama
                                       Gali  Hilo likiwa tayari kwa safari kuelekea  mjini kahama
 Mwili wa Marehemu ukiwa Tayari ndani ya gari la Polisi
 MWILI hapo chini wa marehemu Ezekieli Moshi ukiwa chini  wakati bado taratibu bado zinafanyika za kuusafirisha Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen



KAHAMA
MTU mmoja amefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya kufukiwa na Kifusi katika Shimo walilokuwa wakichimba Dhahabu kwenye Machimbo ya dhahabu yaliyopo katika Kijji cha Ilindi kata ya Zongomera Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo Mkoani Shinyanga, Nicodemas Majaba alisema tukio hilo limetokea jana asubuhi majira ya saa nne ambapo Marehemu huyo alikuwa akichimba dhahabu na wenzake  mara ghafla wakashukiwa na kifusi kilichosababisha kutokea kwa mauaji hayo.

Majaba alimtaja aliyepoteza maisha katika tukio hilo ni Ezekieli Moshi (35) Mkazi wa kijiji cha Mhunze Wilaya ya  Bariadi mkoani Simiyu na wengine wawili  waliojeruhiwa ni Jacob Omoro(35) mkazi wa katoro pamoja na Njile Sospiter (30) mkazi wa bariadi.

Aidha katika hatua nyingine  Majaba alisema kuwa  mashimo hayo yaliyoleta maafa yalikuwa yamesimamishwa kufanya kazi mpaka hapo baaye yatakapotafutiwa  ufumbuzi.

Hata hivyo pamoja na majeruhi hao kulazwa Katika Hospitali  ya Wilaya ya Kahama Mkoani shinyanga Mganga Mfawidhi Joseph Fwoma alisema kuwa hajapata taarifa juu ya Majeruhi hao kulazwa katika hospitali hiyo.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga  kihenya kihenya  alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wachimbaji wachukue tahadhari na kuacha kuchimba dhahabu katika mashimo yasiyokuwa rasmi.
Mwisho.

My Blogger Tricks
blogger

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.