Thursday, November 27, 2014

ajali yaua shinyanga

ajali yaua shinyanga

BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 
Hiace iliyopata ajali ikiwa eneo la tukio huku ikiwa imeharibika vibaya-Picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde
Gari ikiondolewa eneo la tukio
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo akiwa na maafisa wa polisi mkoa wa Shinyanga eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde
WATU tisa wamepoteza maisha   majira ya saa nne na nusu asubuhi kufuatia ajali ya gari ndogo aina ya Hiace yenye namba za usajili T761 CKD lililokuwa  likitoka Kahama kwenda Shinyanga Mjini kupinduka juzi katika eneo la Kona ya Buhangija mjini Shinyanga barabara ya Tinde-Shinyanga.

Mashuhuda wa ajali hiyo walisema gali hilo liilikuwa katika mwendo kasi likifukuzana na Hiace nyingine ndipo ikamshinda dereva wake baada ya kupiga kugonga tuta la Buhangija na kupinduka mara tatu kisha kutumbukia mtaroni.

Mashuhuda wa ajali hiyo waliongeza kusema wameondoa miili mitano ya marehemu katika gari hiyo.

Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga na wanaendelea na matibabu.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt. Mfaume Salum alisema wamepokea miili mitano ya marehemu,na wengine wamefariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali hiyo
 Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Longinus Tibishubwamu abiria waliofariki ni 9 na majeruhi wako 9.

Alisema gari lililopata ajali ni mali ya Fabian Mzaya wa Shinyanga ilikuwa  ikiendeshwa na Anuari Awadhi mkazi  wa Shinyanga aliyekimbia baada ya ajali kutokea.
Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga limedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
HABARI NA KADAMA MALUNDE-SHINYANGA.

My Blogger Tricks
blogger

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.