POLISI MASWA WAWAKERA WANANCHI
Kijana Bundu Kibela(25) akiwa hoi katika hospitali ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu baada ya kupigwa na polisi
Kijana Bundu Kibela(25) akiwa hoi katika hospitali ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu baada ya kupigwa na polisi
JESHI la Polisi wilayani Maswa mkoani Simiyu limewakera wananchi kwa kitendo cha askari wake wawili wenye vyeo vya Police Constebo kumpa kipigo kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Bundu Kibela(25)bila ya kuwa na kosa na hali iliyompelekea kuwa na maumivu makali na kulazwa katika hospitali ya Maswa katika Wodi ya majeruhi.
Kijana huyo inadaiwa kuwa hali yake hairidhishi ambapo anapatiwa chakula kwa kutumia mrija na haja ndogo anatumia mrija.
Askari hao waliokuwa doria siku ya tarehe 22/11/2014 majira ya 1:30 jioni eneo la soko la jioni karibu na mashine ya Msafiri.
Askari hao walikuwa wanne wakike(WP'S wawili)na wa kiume wawili.
Ila mashuhuda walisema kuwa WP'S hawakuhusika kumpiga.
Na baada ya kumaliza kufanya tukio hilo walitumia gari la kiraia kumkimbiza hospitalini lakini walitoa taarifa ya uongo kwa kamanda wa jeshi la Polisi Wilayani humo( OCD) kuwa kijana huyo amepigwa na wananchi wenye hasira kali.
Wananchi Wilayani humo walikuwa wakishuhudia Tukio hilo likifanyika ambapo kilichowaokoa askari hao wasipate kipigo kutoka kwa wananchi hao ni kutokana na kuwa na bunduki mbili aina ya SMG walizokuwa nazo.
Baadhi ya wananchi waliokuwa wakishuudia tukio hilo walisema askari wenye tabia ya kutumia nembo ya polisi vibaya haiwapendezi wananchi kwani sera ya jeshi la polisi ni kuwalinda raia wema na mali zao na si kufanya unyama kwa raia na kwamba huo ni utaratibu wa kizamani wa kikoroni au ni Upolisi wa kizamani wa kupiga raia hovyo hovyo haikubaliki kabisa.
Vitendo hivi ndivyo vinavyowafanya wananchi walichukie jeshi la Polisi hivyo RPC Simiyu na OCD Maswa chukueni hatua.IGP Mangu hakuna haja ya kulea uozo.
HABARI NA SAMWELI MWANGA SIMIYU
|
0 comments:
Post a Comment