HABARI MPYA

Rss

Friday, January 29, 2016
no image

Acacia yatoa msaada wa M.10.5 kwa timu ya Ambassador ya Kahama

Acacia yatoa msaada wa M.10.5 kwa timu ya Ambassador ya Kahama NA PAUL KAYANDA-KAHAMA Januari 29,2016 KAMPUNI ya Acacia kupitia mgodi wake wa Dhahabu Buzwagi umekabidhi hundi ya shilingi Mil.10.5 kuisaidia timu ya Ambasador fc kutoka katika Wilaya ya Kahama Mko wa Shinyanga inayoshiriki ligi daraja la pili ngazi ya mkoa. Akizungumza juzi katika Zoezi la kukabidhi Hundi kwa timu iliyofanyika katika viwanja vya mgodi huo, Meneja mkuu wa mgodi,Assa Mwaipopo aliwapongeza viongozi na wachezaji wa timu hiyo kufikia hatua hiyo na kuwaasa wazidi kuimarisha uongozi ili kuijenga timu yao kufuatia timu nyingi za Tanznaia zikipata misaada kama hiyo kila kiongozi hujali masilahi yake binafsi nakufanya zisikfike mbele. “Hongereni kwa hatua mliyofikia nimeongea na katibu wenu amesema tayari mmefuzu kucheza Fainal mkoani,hiyo ni hatua nzuri ila naomba kuwasii viongozi, kuweni makini katika kuongoza timu yenu na mjitoe kuisadia timu na sio kufanya kazi kwa maslahi yenu binafsi kwakuwa timu imepata fedha hizo japo kidogo”.alisema Meneja. Mwaipopo alitoa ufafanuzi juu ya lengo na dhumuni la kutoa msaada kwa tim hiyo ambayo ipo katika wilaya ya Kahama ambapo ndipo mgodi huo unapofanyanyia shughuli zake za Madini. “Lengo letu kubwa la kutoa msaada huu ni kutaka kuisaidia timu hii likiwa ni lengo la kutekeleza ahadi yetu ya kuisaidia jamii inayotuzunguka,kama mnakumbuka tumetoa udhamini kwa timu ya Stand Utd inayoshiriki Lig kuu ya Vodacom na sasa tumetoa msaada huu wa fedha ili kuisaidia timu hii ifike mbali ifanye vizuri”.alisema Mwaipopo. Nae katibu mkuu wa timu ya Ambasador Bakari Khalid akizungumza kwaniaba ya mkurungezi wa timu hiyo Aray Abeid alitoa shukurani zake kwa kampuni hiyo ya Acacia Buzwagi baada ya kukabidhiwa msaada huo. “Natoa shukrani kwa uongozi mzima Mgodi huu kwa kupokea ombi letu kwaajili ya msaada huu,naomba kuwaahidi kwamba sisi kama Ambasador tutafanya vizuri nakuwa mabalozi wa kuitangaza Kahama katika sekta ya michezo kwani tunao vijana wazuri wenye uwezo wa kucheza mpira na kufanya hivi ni kukuza vipaji vya vijana wetu”alisema Bakari. Timu ya Ambasador fc inayofundishwa na nguli wa zamani katika soka la Tanzania aliewika katika vilabu vya Kahama utd ya zamani ,Pamba ya Mwanza,Moro Utd ya morogoro , klabu ya Yanga ya Dar es salaam na hata katika timu ya taiafa ya Tanzania Taifa Stars Karume Songoro ,ilipata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya timu ya Acacia buzwagi na sasa inajiandaa na faianal ya michuano hiyo ya ligi daraja la pili ngazi ya mkoa inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Wednesday, January 27, 2016
no image

MWANAMKE KAHAMA ASHIKILIWA KWA KUWATUMIKISHA WATOTO KINYUME CHA SHERIA

MTUHUMIWA chiristina andrew mkazi wa nyakato mjini kahama akiwa na mafisa wa uhamiaji kwa mahojiano zaidi juu ya kuwatesa watoto wawili na moja ni raia wa nchini burundi na mwingine ni mkazi wa kibondo mkoani kigoma huku akiwa amefumba machoyake asioneshi uso wake kwenye kamera . YASITA Zakaria 13 akionyesha uso wake ulivyounguazwa kwa maji ya moto na christina andrew kwa kosa la kuchelewa kupika chakula na kuongeza chakula wakati wa kula jioni na kulishwa nyama mbichi kwa maelezo ya yasita amepata mateso makubwa sana. YASITA zakaria 13 mkazi wa mchange nchi burundi akionyeaha majeraha kwenye mgongo wake alivyochumwa na maji ya moto na chirstina andrew32 ni mkazi wa nyakato mjini kahama ambapo ameungua zaidi mwili wake kwa amelezo ya yassita maji hayo yalichemushwa kwenye ente ya maji ya umeme na kisha alimungia mwili wote. AVELINE alobogasti 16 mkazi wa kibondo mkoani kigoma ambaye alikuwa akinya kazi kwa christina andrew nyumbani kwake akionyesha harama za kuchapwa kwa wanya wa umeme na kulishwa nyama bichi na kuchapwa kwa wanya kama jinsi alinaonyesha harama kwenye mkono wake wa afisa wa uhamia ji mjini kahama CHRISTINA Andrew 32 mkazi wa nyakato mjini kahama ambaye anashikiriwa na idara ya uhamiaji kwa kosa la kuajili raia burundi na kuwatesa watoto wawili kwa kuwachoma na maji ya moto mjini kahama MWANAMKE KAHAMA ASHIKILIWA KWA KUWATUMIKISHA WATOTO KINYUME CHA SHERIA. KAHAMA Idara ya uhamiaji wilayani Kahama mkoani Shinyanga inamshikilia Christina Andrew(32)mkazi wa Nyakato mjini Kahama kwa kosa la kuwaajiri na kuwatumikisha kikatili watoto Aveline Alobogasti(16) na Yasinta Zacharia(13) kinyume cha sheria za nchi. Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Afisa Uhamiaji wilayani humo Zacharia Misana alisema mtuhumiwa huyo ameshikiliwa baada ya kubainika kumwajiri Yasinta Zacharia mwenyeji wa Mchange nchini Burundi kitendo ambacho ni kinyume cha sheria za nchi kumwajiri mtu ambaye si raia wa Tanzania.
Friday, December 18, 2015
Wananchi waomba rungu la Magufuli litue  kwa mmiliki wa shule za Kwema kwa kuvamia eneo la wajasiliamali  Kahama

Wananchi waomba rungu la Magufuli litue kwa mmiliki wa shule za Kwema kwa kuvamia eneo la wajasiliamali Kahama

M


       Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawa 

Wananchi waomba rungu la Magufuli litue  kwa mmiliki wa shule za Kwema kwa kuvamia eneo la wajasiliamali  Kahama


KUFUATIA zoezi la bomoabomoa linayoendeelea jijini Dar  es salaam kwa baadhi ya watu wanaojenga katika maeneo ya wazi wilayani Kahama mkoani Shinyanga mfanyabiashara mmoja (Paulin Mathayo) anatuhumiwa kuvamia eneo la wajasiliamali wa viwanda vidogo vidogo (SIDO)kwa kutumia nguvu ya fedha zake.


Mfanya biashara huyo ambaye ni mkurugenzi wa shule ya  msingi Kwema pamoja na Sekondari anatuhumiwa kuvamia eneo la wajasiliamali hao lililopo katika Kata ya Mwendakulima mjini hapa na kujimilikisha bila kufuata sheria na taratibu za Ardhi.


Akiongea na Wandishi wa Habari mwenyekiti wa kikundi cha wajasiliamali hao Charles Omary alisema kuwa eneo hilo walipewa na iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama 1999 kama sehemu yao iliyotengwa kwaajili ya kufanyia shughuli ndogondogo za uchomeleaji vyuma.


Alisema kuwa baada ya kupewa eneo hilo na Halmashauri na kufuata taratibu zote za sheria za Ardhi ikiwa ni pamoja na kulilipia gharama zote za upimaji  sambamba na ulipaji  fidia kwa baadhi ya wananchi waliokuwa wakimiliki mashamba hayo lakini mfanya biashara huyo alivamia na kuanza ujenzi wa shule ya sekondari katika maeneo yao bila kuwashirikisha.


“Eneo hilo tulilipia kwaajili ya kuanza shughuli za uzalishaji mali lakini kwakuwa kulikuwa kunamazao yasiyohamishika ilibidi tukbali ombi la wananchi hadi wavune mazao yao ndipo tulilipie tayari kwa matumizi ya shughuli hizo kwakuwa pia Halmashauri ilituhakikishia kuwa eneo hilo ni mali yetu”.


“Kwa kuona hivyo tuliamua kusubili,lakini katika harakati za kusubili ghafla mfanyabiashara huyo aliamua kuvamia eneo hilo kwa kujenga shule ya sekondari licha ya ku pewa barua ya kusitisha ujenzi wa sekondari hiyo na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya” alisema mwenyekiti huyo Omary.


Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba alipotakiwa kuzungumzia juu ya mgogoro huo alisema kuwa mfanyabiashara huyo yupo kihalali na amepewa hatimiliki sipokuwa eneo hilo wakwanza kupewa ni kikundi hicho cha wajasila mali hivyo weledi unatakiwa kutumika kwa mmoja kuliachia eneo hilo kwa mwenzake.


Hata Msumba alisema kuwa mgogoro huo wa eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 33 yeye ameurithi na kuongeza kuwa hata iliyokuwa Halmashauri iliyokuwapo ilifanya makosa kutoa Hatimiliki kwa mfanyabiashara huyo kwani eneo hilo tayari lilikuwa limekwisha milikiwa na wajasilia mali hao.


“Niwaeleze Wandishi hata viongozi walikuwa halmashauri ya Wilaya ya Kahama ilitumia makosa kutoa hatimiliki kwa mfanyabiashara huyo kwa eneo lililokwisha milikiwa na wajasiliamali hao,hapa sasa inatakiwa weledi utumike ili mmoja wao aliachie eneo hilo atafutiwe lingine huku mfanyabiashara huyo tayari amejenga Sekondari na inatumika,”alisema Msumba.


Hata hivyo kwa upande wake mkurugenzi wa Shule ya awali na shule ya msingi Kwema Paulin Mathayo kila alipotafutwa na vyombo mbalimbali vya Habari amekuwa akimtaka mlinzi kutoruhusu waandishi kuingia ofisini  huku akiwataka waende katika vyombo vya sheria kwa ufafanuzi zaidi.


Habari Na Paul Kayanda-Kahama


Monday, December 14, 2015
 Serikali yawaonya waliovumisha uvujaji wa mitihani kidato cha nne Kahama

Serikali yawaonya waliovumisha uvujaji wa mitihani kidato cha nne Kahama


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgBWqxgQ06ScpScE69x3-L5qz7GNfIVeViMzFLg3Xt94egkSnmCo_lH9Wz8KnJg8H2x2xpggaEOeS7zi-g4Amd_x4bKX0FNZiDRDmvrqcU-J3MuNp6hwnQiNL9YD6LV_avYYnbcIS1Qb8I0/s1600/DSCN9454.JPG



Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga Vita Kawawa akifafanua jambo wakati akizungumza na wandishi wa Habari wilayani hapa juu ya tuhuma zinazowakabili walimu wawili wa shule ya sekondari Anderleck Ridges wanaodaiwa kuhusika katika udanganyifu wa wa mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika Novemba 2015

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgBWqxgQ06ScpScE69x3-L5qz7GNfIVeViMzFLg3Xt94egkSnmCo_lH9Wz8KnJg8H2x2xpggaEOeS7zi-g4Amd_x4bKX0FNZiDRDmvrqcU-J3MuNp6hwnQiNL9YD6LV_avYYnbcIS1Qb8I0/s1600/DSCN9454.JPG
  Picha ya Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Anderleck Ridge Alexander Kazimil ambaye walimu wake wawili wanadaiwa  kuhusika na udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne 2015.

Picha na Maktaba kayandap.blogspot.com.


Serikali yawaonya waliovumisha uvujaji wa mitihani kidato cha nne Kahama

NA PAUL KAYANDA-KAHAMA
Decemba 14, 2014.

SERIKALI Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imetoa onyo kali kwa waliohusika kuzusha taarifa za uongo kupitia vyombo mbalimbali vya Habari nchini  kuwa Walimu Wawili wa Shule ya  Sekondari ya Anderleck Ridge iliyopo Mjini hapa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika novemba2015.


Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa  amesema kuwa  katika Wilaya ya Kahama hakuna kitu kama hicho na kuongeza kuwa Kamati yake ya ulinzi na usalama ilihakikisha ulinzi unaimarishwa kipindi chote cha zoezi hilo na  imemalizika katika hali ya usalama na hakuna Ripoti yeyote iliyowasilishwa kwake kuwa kuna tatizo la uvujaji wa mitihani hiyo.

Amesema taarifa hizo zilizotolewa katika baadhi ya vyombo vya habari kupitia Magazeti ya tarehe 5 Decemba 2015 yalinukuliwa yakiandikwa kuwa walimu wawili wamefikishwa Mahakamani kwa kosa la kukukutwa na mitihani ya kidato cha nne jambo ambalo si la kweli na kuongeza kuwa Mkuu huyo wa Wilaya amesema  Serikali inafanya jitihada za makusudi kuwasaka waliovumisha taarifa hizo.


Kawawa amewataka Wananchi wapuuze uvumi uliotolewa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na tukio hilo kwani ni la upotoshaji likiwa na lengo la kuichafua Serikali pamoja na Watendaji wake na kuongeza kuwa hakuna tukio kama hilo lililoripotiwa katika ofisi yake yeye akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya atahakikisha watu hao wanasakwa hadi wapatikane.

“Ndugu Waandishi wa Habari huo ni uvumi tu, na huyu aliyefanya hivyo sijajua anaugomvi gani na serikali hadi kufikia hatua kusambaza uzushi huo, kwa upande wa kamati ya ulinzi na usalama hali hiyo haikuwapo na watoto walifanya mitihani yao katika hali ya utulivu na amani kila kitengo kiliwasilisha ripoti zake, kamati yangu ya ulinzi na usalama itahakikisha inafuatilia hilo ili kuwabaini wahusika tukiwapata watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo",alisema Kawawa.

Amesema taarifa hizo hazilengi kuichafua shule hiyo bali imelenga kuichafua Serikali pia hivyo hali hiyo siyo ya kufumbiwa macho ni lazima suala hilo lifuatiliwe kwa makini ili waseme ni wapi walikamatwa walimu hao na hadi sasa wapo wapi?,"alihoji Kawawa.

"Hata nyie kama wandishi lazima suala hilo mgelipata mapema na idadi ya wanafunzi mgeijua mbona katika habari zao wanafunzi hawakuhusishwa?kama wamekamatwa Walimu basi hata wanafunzi vilevile wangesitishiwa zoezi la kufanya mitihani hali hii kimsingi siyo nzuri na inalengo baya,"alisema.

Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anastazia Manumbu alisema kuwa katika kipindi chote cha mitihani ya kidato cha nne hakuna tatizo lolote lilijitokeza na kuongeza alikabidhi taarifa ya mitihani katika vyombo husika huku kukiwa hakuna tukio lolote linalohusu Wizi wa mitihani hiyo katika shule zote zilizopo katika Halmashauri Mji huo.

"Baada ya kuupata uvumi huo tuliiachia kamati ya ulinzi ya Wilaya  ifanye uchunguzi wake ili kumbaini mtu huyu na taarifa hiyo kwakweli ilitushtua sana wahusika wa elimu siojui aliyefanya hivo anamakusudi yepi na hata hivyo anatafutwa akipatikana atatusaidia lengo lake ni nini mana yake hakuna mtoto tuliyemkamata na hicho kinachodaiwa wala mwalimu,"alisema Manumbu.

Alisema kuwa baada ya kumalizika mitihani hiyo walisikia uvumi huo ambao kwa upande wake alisema kuwa watu hao walipanga kuwachafua wasimamizi wa mitihani hiyo na kuongeza kuwa kazi hiyo waliiachia kamati ya ulinzi na usalama kufuatilia suala hilo na iwapo kuna mtu atapatikana kuhusika na tuhuma hizo atafikishwa katika vyombo vya sheria.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Anderleck inayotuhumiwa kuhusika na tukio hilo Alexander Kazimiri alisema anapenda kuwaambia Wadau wote kuelewa kuwa suala hilo ni la kupandikizwa na mtu asiyeitakia shule hiyo mema  kwa kutumia fedha zake  kinyume na utaratibu ili kutengeza mazingira ya kuiangamiza taasisi ya Anderleck.

“Mtu huyo atambue kuwa fedha sio kila kitu na ipo siku ataumbuka na wakati mwingine huwa inakwama  na mwisho mtu huyo atapata aibu baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka  sisi tunamwachia Mungu na ukweli wote utabainika baada ya vyombo husika kukamilisha uchunguzi baada ya matokeo kutoka kwani shule yetu wala wanafunzi wetu hawahusiki na kwa namna yeyote ile na udanganyifu wa mitihani bali hizi ni tuhuma tu zisizo na ukweli wowote,"alisema Kazimiri.

Habari iliyoandaliwa na Paul Kayanda,Kahama


Tuesday, October 20, 2015
Mahafari ya saba shule ya sekondari Anderleck;Elimu ndio msingi na mali isiyohamishika;kazimiri

Mahafari ya saba shule ya sekondari Anderleck;Elimu ndio msingi na mali isiyohamishika;kazimiri










Elimu ndio msingi na mali isiyohamishika;kazimiri
  
WAZAZI Nchini wametakiwa kuwakumbusha watoto wao kuwa Elimu ndio msingi na urithi mkubwa wa maisha yao usiohamishika tofauti na kumrisisha Mwanafunzi mali ambazo zinaweza kuisha na kupotea kwa mara moja katika kipindi kifupi.

Hayo alisemwa juzi na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Anderleck Ridges ya Mjini Kahama Alexander Kazimiri katika mahafali ya saba ya kidato cha nne katika Sekondari hiyo yalifanyika Mjini hapa na kusisitiza kuwa Elimu ndio msingi wa maisha kwa sasa.

Kazimiri alisema kuwa kitendo cha wazazi kuwarisisha Watoto wao mali badala ya Elimu ni kuwapotosha kwani mali hizo zinaweza kupotea wakati wowote na kusababisha Umasikini mkubwa katika familia.

“Kwa sasa katika jamii suala la Elimu ni muhimu kwa watoto lakini Elimu hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwa ni sambamba na mmomonyoka mkubwa wa maadili unaochangiwa na mitandao inayotumiwa na watoto wetu”, Alisema Alexandaer Kazimiri Mkurugenzi wa Shule yaSekondari ya Anderleck Ridges.

Aidha Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa Elimu kwa sasa inatakiwa kutolewa kuendana hali iliyopo ya sayansi na Teknolojia lakini imekuwa ikitumika vibaya katika kupotosa Watoto hususani wanafunzi ambao muda wao mwingi wanaupoteza katika masuala ya kuwasiliana kwa njia ya mtandao.

Hata hivyo Kazimiri hakusita katika kulaani mauwaji ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (Albino) na kuongeza kuwa mauwaji hayo yamekuwa yakifanyika kutokana na watu kukosa Elimu kwa kiasi kikubwa.


“Kwa sasa tunashuku mungu kuona hali hiyo ya mauwaji imeweza kupungua kwa kiasi kikubwa katika Mkoa wa Shinyanga na sasa hatuna budi kuendelea kutoa Elimu juu ya kukomesha kabisa hali hiyo na yasiweze kutokea tena katika siku za baadaye”, Aliongeza Kazimiri.

Katika mahafali hayo ya saba katika Shule hiyo, jumla ya wanafunzi 164 walifanikiwa kuhitimu masomo ya kidato cha nne katika shule hiyo huku idadi ya wanafunzi wa kike wakiwa 42 hali ambayo bado inaleta changamoto kwa wazazi kuwapeleka watoto hao wa kike kwa wingi shuleni ili waweze kupata elimu.

Habari na Paul Kayanda, Kahama


Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.