Wananchi waomba rungu la Magufuli litue kwa mmiliki wa shule za Kwema kwa kuvamia eneo la wajasiliamali Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawa
Wananchi
waomba rungu la Magufuli litue kwa mmiliki wa shule za Kwema kwa kuvamia
eneo la wajasiliamali Kahama
KUFUATIA zoezi la bomoabomoa linayoendeelea jijini Dar es salaam kwa baadhi ya watu wanaojenga katika maeneo ya wazi wilayani Kahama mkoani Shinyanga mfanyabiashara mmoja (Paulin Mathayo) anatuhumiwa kuvamia eneo la wajasiliamali wa viwanda vidogo vidogo (SIDO)kwa kutumia nguvu ya fedha zake.
Mfanya
biashara huyo ambaye ni mkurugenzi wa shule ya msingi Kwema pamoja na
Sekondari anatuhumiwa kuvamia eneo la wajasiliamali hao lililopo katika Kata ya
Mwendakulima mjini hapa na kujimilikisha bila kufuata sheria na taratibu za
Ardhi.
Akiongea
na Wandishi wa Habari mwenyekiti wa kikundi cha wajasiliamali hao Charles Omary
alisema kuwa eneo hilo walipewa na iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama
1999 kama sehemu yao iliyotengwa kwaajili ya kufanyia shughuli ndogondogo za
uchomeleaji vyuma.
Alisema
kuwa baada ya kupewa eneo hilo na Halmashauri na kufuata taratibu zote za
sheria za Ardhi ikiwa ni pamoja na kulilipia gharama zote za upimaji
sambamba na ulipaji fidia kwa baadhi ya wananchi waliokuwa wakimiliki
mashamba hayo lakini mfanya biashara huyo alivamia na kuanza ujenzi wa shule ya
sekondari katika maeneo yao bila kuwashirikisha.
“Eneo
hilo tulilipia kwaajili ya kuanza shughuli za uzalishaji mali lakini kwakuwa
kulikuwa kunamazao yasiyohamishika ilibidi tukbali ombi la wananchi hadi wavune
mazao yao ndipo tulilipie tayari kwa matumizi ya shughuli hizo kwakuwa pia
Halmashauri ilituhakikishia kuwa eneo hilo ni mali yetu”.
“Kwa
kuona hivyo tuliamua kusubili,lakini katika harakati za kusubili ghafla
mfanyabiashara huyo aliamua kuvamia eneo hilo kwa kujenga shule ya sekondari
licha ya ku pewa barua ya kusitisha ujenzi wa sekondari hiyo na uongozi wa
Halmashauri ya Wilaya” alisema mwenyekiti huyo Omary.
Naye
mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba alipotakiwa
kuzungumzia juu ya mgogoro huo alisema kuwa mfanyabiashara huyo yupo kihalali
na amepewa hatimiliki sipokuwa eneo hilo wakwanza kupewa ni kikundi hicho cha
wajasila mali hivyo weledi unatakiwa kutumika kwa mmoja kuliachia eneo hilo kwa
mwenzake.
Hata
Msumba alisema kuwa mgogoro huo wa eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 33 yeye
ameurithi na kuongeza kuwa hata iliyokuwa Halmashauri iliyokuwapo ilifanya
makosa kutoa Hatimiliki kwa mfanyabiashara huyo kwani eneo hilo tayari lilikuwa
limekwisha milikiwa na wajasilia mali hao.
“Niwaeleze
Wandishi hata viongozi walikuwa halmashauri ya Wilaya ya Kahama ilitumia makosa
kutoa hatimiliki kwa mfanyabiashara huyo kwa eneo lililokwisha milikiwa na
wajasiliamali hao,hapa sasa inatakiwa weledi utumike ili mmoja wao aliachie
eneo hilo atafutiwe lingine huku mfanyabiashara huyo tayari amejenga Sekondari
na inatumika,”alisema Msumba.
Hata
hivyo kwa upande wake mkurugenzi wa Shule ya awali na shule ya msingi Kwema
Paulin Mathayo kila alipotafutwa na vyombo mbalimbali vya Habari amekuwa
akimtaka mlinzi kutoruhusu waandishi kuingia ofisini huku akiwataka
waende katika vyombo vya sheria kwa ufafanuzi zaidi.
Habari Na Paul Kayanda-Kahama
0 comments:
Post a Comment