Friday, January 29, 2016

Acacia yatoa msaada wa M.10.5 kwa timu ya Ambassador ya Kahama

Acacia yatoa msaada wa M.10.5 kwa timu ya Ambassador ya Kahama NA PAUL KAYANDA-KAHAMA Januari 29,2016 KAMPUNI ya Acacia kupitia mgodi wake wa Dhahabu Buzwagi umekabidhi hundi ya shilingi Mil.10.5 kuisaidia timu ya Ambasador fc kutoka katika Wilaya ya Kahama Mko wa Shinyanga inayoshiriki ligi daraja la pili ngazi ya mkoa. Akizungumza juzi katika Zoezi la kukabidhi Hundi kwa timu iliyofanyika katika viwanja vya mgodi huo, Meneja mkuu wa mgodi,Assa Mwaipopo aliwapongeza viongozi na wachezaji wa timu hiyo kufikia hatua hiyo na kuwaasa wazidi kuimarisha uongozi ili kuijenga timu yao kufuatia timu nyingi za Tanznaia zikipata misaada kama hiyo kila kiongozi hujali masilahi yake binafsi nakufanya zisikfike mbele. “Hongereni kwa hatua mliyofikia nimeongea na katibu wenu amesema tayari mmefuzu kucheza Fainal mkoani,hiyo ni hatua nzuri ila naomba kuwasii viongozi, kuweni makini katika kuongoza timu yenu na mjitoe kuisadia timu na sio kufanya kazi kwa maslahi yenu binafsi kwakuwa timu imepata fedha hizo japo kidogo”.alisema Meneja. Mwaipopo alitoa ufafanuzi juu ya lengo na dhumuni la kutoa msaada kwa tim hiyo ambayo ipo katika wilaya ya Kahama ambapo ndipo mgodi huo unapofanyanyia shughuli zake za Madini. “Lengo letu kubwa la kutoa msaada huu ni kutaka kuisaidia timu hii likiwa ni lengo la kutekeleza ahadi yetu ya kuisaidia jamii inayotuzunguka,kama mnakumbuka tumetoa udhamini kwa timu ya Stand Utd inayoshiriki Lig kuu ya Vodacom na sasa tumetoa msaada huu wa fedha ili kuisaidia timu hii ifike mbali ifanye vizuri”.alisema Mwaipopo. Nae katibu mkuu wa timu ya Ambasador Bakari Khalid akizungumza kwaniaba ya mkurungezi wa timu hiyo Aray Abeid alitoa shukurani zake kwa kampuni hiyo ya Acacia Buzwagi baada ya kukabidhiwa msaada huo. “Natoa shukrani kwa uongozi mzima Mgodi huu kwa kupokea ombi letu kwaajili ya msaada huu,naomba kuwaahidi kwamba sisi kama Ambasador tutafanya vizuri nakuwa mabalozi wa kuitangaza Kahama katika sekta ya michezo kwani tunao vijana wazuri wenye uwezo wa kucheza mpira na kufanya hivi ni kukuza vipaji vya vijana wetu”alisema Bakari. Timu ya Ambasador fc inayofundishwa na nguli wa zamani katika soka la Tanzania aliewika katika vilabu vya Kahama utd ya zamani ,Pamba ya Mwanza,Moro Utd ya morogoro , klabu ya Yanga ya Dar es salaam na hata katika timu ya taiafa ya Tanzania Taifa Stars Karume Songoro ,ilipata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya timu ya Acacia buzwagi na sasa inajiandaa na faianal ya michuano hiyo ya ligi daraja la pili ngazi ya mkoa inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
My Blogger Tricks
blogger
Next
This is the most recent post.
Older Post

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.