Serikali yawaonya waliovumisha uvujaji wa mitihani kidato cha nne Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga Vita Kawawa akifafanua jambo wakati akizungumza na wandishi wa Habari wilayani hapa juu ya tuhuma zinazowakabili walimu wawili wa shule ya sekondari Anderleck Ridges wanaodaiwa kuhusika katika udanganyifu wa wa mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika Novemba 2015
Picha ya Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Anderleck Ridge Alexander Kazimil ambaye walimu wake wawili wanadaiwa kuhusika na udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne 2015.
Picha na Maktaba kayandap.blogspot.com.
Serikali yawaonya waliovumisha
uvujaji wa mitihani kidato cha nne Kahama
NA PAUL KAYANDA-KAHAMA
Decemba 14, 2014.
SERIKALI Wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga imetoa onyo kali kwa waliohusika kuzusha taarifa za uongo kupitia
vyombo mbalimbali vya Habari nchini kuwa
Walimu Wawili wa Shule ya Sekondari ya
Anderleck Ridge iliyopo Mjini hapa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika novemba2015.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita
Kawawa amesema kuwa katika Wilaya ya Kahama hakuna kitu kama
hicho na kuongeza kuwa Kamati yake ya ulinzi na usalama ilihakikisha ulinzi unaimarishwa kipindi chote cha zoezi hilo na imemalizika katika hali ya usalama na hakuna Ripoti yeyote
iliyowasilishwa kwake kuwa kuna tatizo la uvujaji wa mitihani hiyo.
Amesema taarifa hizo zilizotolewa
katika baadhi ya vyombo vya habari kupitia Magazeti ya tarehe 5 Decemba 2015
yalinukuliwa yakiandikwa kuwa walimu wawili wamefikishwa Mahakamani kwa kosa la
kukukutwa na mitihani ya kidato cha nne jambo ambalo si la kweli na kuongeza
kuwa Mkuu huyo wa Wilaya amesema Serikali inafanya jitihada za makusudi kuwasaka
waliovumisha taarifa hizo.
Kawawa amewataka Wananchi wapuuze
uvumi uliotolewa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na tukio hilo kwani ni
la upotoshaji likiwa na lengo la kuichafua Serikali pamoja na Watendaji wake na
kuongeza kuwa hakuna tukio kama hilo lililoripotiwa katika ofisi yake yeye akiwa
kama Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya atahakikisha watu hao wanasakwa hadi wapatikane.
“Ndugu Waandishi wa Habari
huo ni uvumi tu, na huyu aliyefanya hivyo sijajua anaugomvi gani na serikali hadi kufikia hatua kusambaza uzushi huo, kwa upande wa kamati ya ulinzi na usalama hali hiyo haikuwapo na watoto walifanya mitihani yao katika hali ya utulivu na amani kila kitengo kiliwasilisha ripoti zake, kamati yangu ya ulinzi na usalama itahakikisha inafuatilia hilo ili kuwabaini wahusika tukiwapata watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo",alisema Kawawa.
Amesema taarifa hizo hazilengi kuichafua shule hiyo bali imelenga kuichafua Serikali pia hivyo hali hiyo siyo ya kufumbiwa macho ni lazima suala hilo lifuatiliwe kwa makini ili waseme ni wapi walikamatwa walimu hao na hadi sasa wapo wapi?,"alihoji Kawawa.
"Hata nyie kama wandishi lazima suala hilo mgelipata mapema na idadi ya wanafunzi mgeijua mbona katika habari zao wanafunzi hawakuhusishwa?kama wamekamatwa Walimu basi hata wanafunzi vilevile wangesitishiwa zoezi la kufanya mitihani hali hii kimsingi siyo nzuri na inalengo baya,"alisema.
Kwa upande wake Afisa Elimu
Sekondari wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anastazia Manumbu alisema kuwa katika
kipindi chote cha mitihani ya kidato cha nne hakuna tatizo lolote lilijitokeza
na kuongeza alikabidhi taarifa ya mitihani katika vyombo husika huku kukiwa
hakuna tukio lolote linalohusu Wizi wa mitihani hiyo katika shule zote zilizopo
katika Halmashauri Mji huo.
"Baada ya kuupata uvumi huo tuliiachia kamati ya ulinzi ya Wilaya ifanye uchunguzi wake ili kumbaini mtu huyu na taarifa hiyo kwakweli ilitushtua sana wahusika wa elimu siojui aliyefanya hivo anamakusudi yepi na hata hivyo anatafutwa akipatikana atatusaidia lengo lake ni nini mana yake hakuna mtoto tuliyemkamata na hicho kinachodaiwa wala mwalimu,"alisema Manumbu.
Alisema kuwa baada ya kumalizika
mitihani hiyo walisikia uvumi huo ambao kwa upande wake alisema kuwa watu hao
walipanga kuwachafua wasimamizi wa mitihani hiyo na kuongeza kuwa kazi hiyo
waliiachia kamati ya ulinzi na usalama kufuatilia suala hilo na iwapo kuna mtu
atapatikana kuhusika na tuhuma hizo atafikishwa katika vyombo vya sheria.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Shule ya
Sekondari ya Anderleck inayotuhumiwa kuhusika na tukio hilo Alexander Kazimiri
alisema anapenda kuwaambia Wadau wote kuelewa kuwa suala hilo ni la
kupandikizwa na mtu asiyeitakia shule hiyo mema
kwa kutumia fedha zake kinyume na
utaratibu ili kutengeza mazingira ya kuiangamiza taasisi ya Anderleck.
“Mtu huyo atambue kuwa fedha sio
kila kitu na ipo siku ataumbuka na wakati mwingine huwa inakwama na mwisho mtu huyo atapata aibu baada ya
matokeo ya kidato cha nne kutoka sisi
tunamwachia Mungu na ukweli wote utabainika baada ya vyombo husika kukamilisha
uchunguzi baada ya matokeo kutoka kwani shule yetu wala wanafunzi wetu hawahusiki na kwa namna yeyote ile na udanganyifu wa mitihani bali hizi ni tuhuma tu zisizo na ukweli wowote,"alisema Kazimiri.
Habari iliyoandaliwa na Paul Kayanda,Kahama
0 comments:
Post a Comment