Serikali yatakiwa kutoa ruzuku kwa shule binafsi
Kaim mkurugenzi wa shule ya sekondari mwalimu Tutuba akiwa ofisini kwakeBaadhi ya madarasa ya shule hiyo
Jengo la utawala la ofisi ya shule ya sekondari mwalimu Tutuba
Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule hiyo wakiomba kujibu maswali yanayoulizwa na mwalimu wa darasa
Moja ya nembo ya shule ya sekondari mwalimu Tutuba iliyopo Kibondo mkoani Kigoma.
WADAU na Wamiliki wa Shule binafsi za Sekondari Wilayani Kibondo
Mkoa wa Kigoma wameiomba Serikali kutoa Ruzuku kwa shule hizo ili kuweza
kuhimili grarama za uendeshaji na kukuza sekta ya Elimu hapa nchini.
Wakizungumza juzi na Gazeti hili Wadau hao walisema kuwa iwapo
Serikali itatoa Ruzuku kwa shule binafsi suala la Elimu hapa nchini litakuwa ni
rahisi sana kwani kutakuwa na ushirikiano mkubwa baina ya pande hizo
mbili, Serikali na wamiliki binafsi wa shule hizo.
Mmoja wa Wamiliki wa Shule moja binafsi ya sekondari Mwalimu
Tutuba ya mjini Kibondo Salehe Makunga alisema kuwa kwa sasa baadhi ya shule za
sekondari zinazomilikiwa na watu binafsi zimekuwa hazifanyi vizuri kutokana na
wamiliki wake kutokuwa na mitaji inayotosha uendeshaji wa shule hizo.
Aidha Makunga alisema kuwa kumekuwa na matatizo mbalimbali ambayo
yamekuwa yakizikabili shule hizo kama vile kutokuwa na maabara kwa ajili
kusomea wanafunzi masomo ya Sayansi na pia upungufu wa majengo hali ambayo kama
serikali ingekuwa inatoa Ruzuku kungekuwa ahueni katika kufanikisha
ukamilishaji wa mapungufu hayo.
Aidha Mwalimu Makunga alisema kuwa kutokana na changamoto zilizopo
katika shule hizo hususani shule yake, lakini shule yake imejiwekea malengo
makubwa ya kuboresha majengo yake pamoja ukamilishwaji wa vyumba vya maara hadi
kufikia mwaka 2020.
“Tunashindwa kuboresha baadhi ya majengo katika shule hii kutokana
na fedha nyingi tunategemea kutoka kwa wazazi hali ambayo mpaka kufikia hivi
sasa hatuna fedha kwani hata hao wazazzi wanategemea kupata fedha zinazotokana
na shughuli za kilimo wanazofanya hali ambayo inakuwa ni vigumu kuendeleza
shule”,Alisema Makunga.
Pia Mwalimu huyo hakusita kuwalaumu baadhi ya wazazi katika Wilaya
ya Kibondo kwa kutokuwa mstari wa mbele katika kuwasomesha watoto wao hasa
katika Elimu ya Sekondari hata Pindi wanapofauli darasa la saba hali ambayo
inachangia kuwa na mrundikano wa watoto ambao hawajapata elimu ya sekondari kwa
kiwango kikubwa.
Kwa upande wake Mwalimu wa Taaluma katika shule hiyo Amos Kilagambalaye
alisema kuwa pamoja na shule hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni
pamoja na serikali kuzisahau shule binafsi na kujikita na shule za serikali
lakini shule hiyi imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya kiwilaya hadi
kimkoa kwa muda miaka miwili iliyopita.
Kilagambalaye aliwapongeza Wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo
kwa kuwa wasikivu pamoja na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha
masomo hali ambayo inawatia moyo hata Walimu na wazazi wanaopenda Elimu katika
Wilaya hiyo.
“Tumekuwa pia tukifanya vizuri kutoka na ushirikiano mkubwa uliopo
baina ya shule hii pamoja na shule zingine zinazofanya vizuri hapa
nchini kama vile St Marys ya Jijini Dare es Salaam hali ambayo inatuongerzea
morari wa kuendelea kufanya vizuri siku za baadaye”, Alisema Mwalimu huyo wa
Taaluma wa shule ya sekondari Mwalimu Tutuba.
Habari PAUL KAYANDA-KIGOMA
0 comments:
Post a Comment