Saturday, July 11, 2015

Dc Nyang’wale Atishia kuhamisha kijiji

 Wchimbaji wadogo wakiwa katika mazungumzo na wandishi wa Habari waliotembelea machimbo hayo.

Wachimbaji wadogo wa machimbo ya Ng'wasabuka yaliyopo kkitongoji cha Iyenze kata ya Mwingilo Wilaya ya Nyang'wale mkoani Geita wakiwa katika hali ya sintofahamu kulingana na mkuu wa Wilaya hiyo kuwatishia kuleta jeshi la Polisi kwa lengo la kuwaondoa kwa nguvu
Wakati huo wengine wakiendelea kuipuuza hali hiyo na kuendelea na majukumu yao huku wengine wakibeba viroba vya mchanga vyenye chembechembe ya dhahabu.
 Wchimbaji hao wakiwa sehemu yao ya kazi.
 MKUU wa Wilaya ya Nyanang’wale  mkoani Geita Ibrahimu Malwa ametishia kuwahamisha wakazi wa kijiji cha Ng’wasabuka kitongoji cha  Iyenze kata ya Mwigilo kilichopo mkoani humo kwa kile kinachodaiwa kuwepo kwa machimbo mapya ya Madini ya Dhahabu yaliyoibuliwa na wachimbaji  wadodo wadogo.
 
Malalamiko hayo yalitolewa juzi kwa waandishi wa Habari waliofika machimboni hapo na wachimbaji wadogo wadogo wa eneo hilo na kuitupia lawama Serikali  ambapo kila wanapoibua machimbo mapya huvamiwa na Serikali  kwa madai kuwa maeneo hayo ni mali ya wawekezaji wakubwa.
Mmoja wa wachimbaji hao Charles Kapngo alisema kuwa wamekuwa wakipokea viisho toka kwa Jeshi laPolisi wilayani humo wanaotumiwa na mkuu wa Wilaya hiyo Ibrahimu Malwa likiwataka kuondoka kweye eneo hilo linalodaiwa kuwa ni mali ya mwekezaji wa kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi wa Bulyanhulu.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Ibrahimu Malwa alipohojiwa kuhusiana na hali hiyo alisema wachimbaji hao wanaendesha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo kinyume cha sheria za Madini na kuongea kuwa eneo wanalochima ni leseni ya mwekezaji wa kampuni ya Acacia endapo watakaidi wataondolewa kwa nguvu.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema wachimbaji hao aliwapa muda wa mwezi mmoja wawe wamehama na alitoa muda huo kulingana na malalamiko yao waliyoyapeleka kwake baada ya mwekezaji huyo kuwataka waondoke  katika eneo hilo  na kuongeza kuwa hata hivyo wanaonekana kukaidi agizo hilo.
Naye afisa mawasiliano wa kampui ya Acacia Mary Lupamba alipotakiwa kutoa ushirikiano wa suala hilo alimtaka mwandishi wa Habari hizi amtafute mkuu wa Wilaya hiyo kwani ndiye mwenye majibu sahihi kutokana kwamba yeye ni kiongozi wa Serikali.
Afisa madini Mkoa wa Geita Musimu Kabasa alisema walifanya mkutano wa pamoja na wachmbaji hao sambamba na mwekezaji na uongozi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya hiyo na kukubaliana na wachimbaji hao kutoka eneo hilo ndani ya mwezi mmoja lakini walikimbilia tena kwa viongoziwa siasa.
Wachimbaji hao walisema kuwa kutokana na hapo awali uzalishaji ulipokuwa upo juu mkuu wa ilaya hiyo pamoja na Afisa huyo wa Madini walikuwa na maduara yao  na walikuwa wakipewa pesa mara kwa mara hivyo uzalishaji ulipo shuka ndipo waliamua kuwageuka wachimbaji hao.

Kiongozi wa wachimbaji hao Charles Kapongo mwenye kofia ya duara na suti nyeusakiangalia hali ya mazingira ya mgodi huo huku akiwa na hofu kwamba Jeshi la Polisi linaweza kuingia muda wowote.

Hii ndiyo hali halisi ilivyo ndani ya machimbo hayo waliyoibua wachimbaji wadogowadogo huko Nyang'wale Geita

Wandishi wa Habari wa magazeti ya Habari leo na Majira Raymond Mihayo na Shaban Njia wakizuru mazingira ya machimbo hayo huku wakiwa na meneja wa Machimbo hayo Bw. Ngulyati.
 Wachimbaji hao wakiteta jambo na wandishi wa Habari waliofika mazingira hayo.
 
    Dc Nyang’wale Atishia kuhamisha kijiji

MKUU wa Wilaya ya Nyanang’wale  mkoani Geita Ibrahimu Malwa ametishia kuwahamisha wakazi wa kijiji cha Ng’wasabuka kitongoji cha  Iyenze kata ya Mwigilo kilichopo mkoani humo kwa kile kinachodaiwa kuwepo kwa machimbo mapya ya Madini ya Dhahabu yaliyoibuliwa na wachimbaji  wadodo wadogo.

Malalamiko hayo yalitolewa juzi kwa waandishi wa Habari waliofika machimboni hapo na wachimbaji wadogo wadogo wa eneo hilo na kuitupia lawama Serikali  ambapo kila wanapoibua machimbo mapya huvamiwa na Serikali  kwa madai kuwa maeneo hayo ni mali ya wawekezaji wakubwa.

Mmoja wa wachimbaji hao Charles Kapongo alisema kuwa wamekuwa wakipokea viisho toka kwa Jeshi laPolisi wilayani humo wanaotumiwa na mkuu wa Wilaya hiyo Ibrahimu Malwa likiwataka kuondoka kweye eneo hilo linalodaiwa kuwa ni mali ya mwekezaji wa kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi wa Bulyanhulu.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Ibrahimu Malwa alipohojiwa kuhusiana na hali hiyo alisema wachimbaji hao wanaendesha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo kinyume cha sheria za Madini na kuongea kuwa eneo wanalochima ni leseni ya mwekezaji wa kampuni ya Acacia endapo watakaidi wataondolewa kwa nguvu.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema wachimbaji hao aliwapa muda wa mwezi mmoja wawe wamehama na alitoa muda huo kulingana na malalamiko yao waliyoyapeleka kwake baada ya mwekezaji huyo kuwataka waondoke  katika eneo hilo  na kuongeza kuwa hata hivyo wanaonekana kukaidi agizo hilo.

Naye afisa mawasiliano wa kampui ya Acacia Mary Lupamba alipotakiwa kutoa ushirikiano wa suala hilo alimtaka mwandishi wa Habari hizi amtafute mkuu wa Wilaya hiyo kwani ndiye mwenye majibu sahihi kutokana kwamba yeye ni kiongozi wa Serikali.
Afisa madini Mkoa wa Geita Musimu Kabasa alisema walifanya mkutano wa pamoja na wachmbaji hao sambamba na mwekezaji na uongozi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya hiyo na kukubaliana na wachimbaji hao kutoka eneo hilo ndani ya mwezi mmoja lakini walikimbilia tena kwa viongoziwa siasa.

Wachimbaji hao walisema kuwa kutokana na hapo awali uzalishaji ulipokuwa upo juu mkuu wa ilaya hiyo pamoja na Afisa huyo wa Madini walikuwa na maduara yao  na walikuwa wakipewa pesa mara kwa mara hivyo uzalishaji ulipo shuka ndipo waliamua kuwageuka wachimbaji hao.

Habari na Paul Kayanda-Geita

My Blogger Tricks
blogger

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.