MAHAFARI YA KWNAZA YA DARASA LA SBA SUNSET
CAPTAIN Omary Hanzuruni akiwaongoza mgeni rasmi katika mahafari hayo,Zacharia Misana Afisa uhamiaji Wilayani Kahama pamoja na Mkurugenzi wa mji wa Kahama, Felix Kimaryo kwenda kukagua gwalide la vijana kutoka shule ya msingi SunsetMlezi wa shule ya Sunset, Mahamoud Jaha kulia akiwa sambamba na Afisa uhamiaji ,Zacharia Misana wakiongozwa na captain Hanzuruni kuelekea jukwaa la vijana machachari katika kuhakikisha wanamazoezi mazuri ya kulinda Taifa
Vijana wa kikosi kutoka Shule ya Sunset wakiwa wamejipanga kikakamavu
Viongozi hao wakisindikizwa na mlezi wa Shule hiyo wakiwakagua maaskari hao kuona shughuli za kiusalama zinatimizwa vizuri
Captain Hanzurini akiwatambulisha maaskari wake kwa wakaguzi wa vikosi hivyo
Twendeni na huku muone
Afisa huyo wa Uhamiaji mwenyesuti ya kaki pamoja na mlezi wa shule hiyo wakiwa wamesimama kikakamavu huku wakiangalia kama maaskari hao wako sawa
Hili ni jeshi la JKT likiwa tayari kwa lolote
Wakiangalia jeshi la Magereza mchanganyiko na la Uhamiaji kwa makini
Simama imara
Katiza uone cha moto
Captain Hanzuruni akiwa mbele ya maaskari wake
TUPO IMARA
Jeshi la majini likionyesha umahili wake kazini
Waogope hao
Wakiwa tayari kukabiliana na maadui
Wakipita huku macho nyuma nakusonga mbele bila kupindisha mistari
Wakiwa katika mwendo wa haraka
Walimu wakiwa pamoja na wanafunzi wao
Mlezi wa Shule ya Sunset Mahamoud Jaha mweye suti ya blauni akiw na skafu shingoni kushoto kwake ni Afisa Uhamiaji akiwa wa Wilaya ya Kahama, Zacharia Misana, mwenyekaundasuti ni Mkurugenzi wa mji wa Kahama,Felix kimaryo wakiwa meza kuuu wakiwatazama wanafunzi wa shule hiyo wakati wakionyesha maonyesho ya jeshi la ulinzi yaliyoandaliwa na shule hiyo.
Baadhi ya walimu kutoka shule mbalimbali za watu binafsi wilayani humo
WAKILITAWALA JUKWAA
Wapiga bendi la gwalide mahili wa shule hiyo
Jinsi palivyokuwa
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa katika picha na kwenye mahafali hayo
TUMEPENDEZA
USITUSOGELEE
TUNAPIGA PICHA
TUMEMALIZA DARASA LA SABA TUKIW NA AFYA NZURI TUMEFURAHI
UKITUONA TUPO KAZINI PIT MBALI CHEZEA SIRAHA WEWE
Maaskari hawa wamepata nafasi ya kuzungumza na blog hiii na kusema kuwa hata wakifanikiwa kuingia katika kidato cha sita hapo baadye mungu akipenda watajiunga na jeshi la kulinda Taifa JKT na kuahidi kulitumikia taifa hili vyema.
Hiki ni kikosi cha makomando wa Tanzania wakionyesha umahili wao wa kung'fuu mbele ya viongozi wao pamoja na mgeni rasmi
Komando akimkabili adui
kikundi cha kwaya cha shule hiyo
Wanakwaya wakiwa wamependeza huku wakiimba kwa kuringa na kujidai kwa nyimbo yao nzuri
Kikundi cha ngoma asili kilichoandaliwa na meneja wa shule ya msingi Sunset,Nadine Mahamoud
Tunajivunia kusoma katika shule nzuri yenye walimu waliobobea kwa masomo ya kiingereza pamoja na Computer
Kikundi cha makabila ya wahaya kwa kina pacha wa Saida kalolo kilichoratibiwa na Meneja huyo Sunset kilisisimua watu waliohudhulia mahafari hayo hali iliyowalazimu makabila mbalimbali kwenda kucheza na kulishambulia jukwaa hilo
Kikundi cha wahaya kilichoibua hisia za mamia ya watu waliohudhulia mahafari hayo kililitawala jukwaa hilo
wananchi wengi kanda ya ziwa hawathamini elimu
IMEELEZWA
kuwa kitendo cha Wananchi wengi waliopo katika kanda ya ziwa kutokuthamini
Elimu kwa kiasi kikubwa kimesababisha baadhi ya fursa nyingi zilizopo katika
kanda hiyo hasa katika Migodi huchukuliwa na watu kutoka katika mikoa mingine
iliyopo nje na migodi hiyo.
Hayo
yalisemwa juzi na Afisa wa uhamiaji wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga,Zacharia Missana katika
Mahafali ya kwanza ya shule ya msingi Sunset yalifanyika mjini Kahama na
kuongeza kuwa kwa sasa watu wa maeneo hayo lazima wabadilike.
Missana
alisema kuwa katika Dunia ya sasa huwezi
kupata hata fursa ya kufanya kazi katika Migodi iliyopo katika Wilaya ya Kahama
bila ya kuwa na Elimu ya kutosha hali ambayo kwa wananchi wa maeneo hayo
wamekuwa wakilalamika juu ya kukosa fursa za kupata kazi katika maeneo hayo ya
migodi nakwamba wanatakiwa kujua elimu
ndio kipaumbele.
Afisa
Uhamiaji huyo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya
katika Mahafali hayo alisema kuwa kwa sasa wanachi wa maeneo hayo hawana budi kushirikiana
na wawekezaji waliopo katika Wilaya ya Kahama katika masuala mazima yanayohusu
Elimu ili iwe rahisi katika kufanikisha uhamasishaji wa elimu.
Aliwataka
Wakazi wa Kahama kuamka katika suala zima la Elimu na kuongeza kuwa hata
mauwaji ya vikongwe yalioshamiri katika maeneo ya wilaya ya Kahama na Mkoa wa
Shinyanga kwa ujumla yanaweza kuisha kama kila mtu atakuwa na Elimu ya kutosha
na kuwa msaada mkubwa kwa wengine.
Kwa
upande wake Mlezi wa Shule ya Sunset Mahamoudu Jaha alisema kuwa suala la Elimu
katika dunia ya sasa sio la kubeza na kuishauri serikali kuzidi kuboresha miundo
mbinu kwa kiasi kikubwa suala la elimu ili kila Mtanzania aweze kusoma na
kusomesha watoto bila ya kuwa na malalamiko yeyote.
Nae
Mkuu wa Shule hiyo Eliasafu Bayaga katika risala yake aliyoisoma mbele ya mgeni rasmi katika
mahafari hayo alisema kuwa shule hiyo
ilianza mwaka 2010 na kuwashauri wazazi kuwatunza wanafunzi majumbani kwao kwa
nidhamu wakati wakisubiri matokeo yao hali ambayo itawafanya kuingia kidato cha
kwanza wakiwa katika maadili mema.
Shule
ya Sunset iliyopo mjini Kahama jumla ya Wanafunzi 23 walihitimu darasa la saba
huku wanafunzi 13 wa shule ya awali wakifanikiwa kupata vyeti vya kujiunga na
darasa la kwanza kwa mwaka ujao katika shule hiyo.
PAUL KAYANDA-KAHAMA SHINYANGA,
0 comments:
Post a Comment