Bugarama watakiwa kuliombea amani Taifa hili katika kipindi kijacho cha uchaguzi
- Gari zilizotumika siku ya Uzinduzi wa albamu hiyo
Diwani wa Kata ya bugarama Nixson Igoko mwenyekaunda suti na mwenye shati jeupe ni mwenyekiti wa kijiji cha Bugarama Jimmy Kemano wakiketi pamoja siku ya uzinduzi
Wnanchi wa kijiji cha Bugarama wakiangalia kwa makini michezo mbalimbali siku ya uzinduzi huo wa niymbo za Injili zilizofanyika kati viwanja vya kanisa la EAGT bugarama
Wanakwaya wa kanisa katoliki Bugarama wakiimba nyimbo za kusifu uzinduzi huo
Migizaji katika siku hiyo akiwafurahisha wananchi waliohudhuria siku hiyo
Mwenyekiti huyo wa kijiji jimmy Kemano akifurahi na wageni wenzake walioarikwa sikua hiyo baada ya wasaniii wa maigizo kuzidi kukoleza kwa vichekesho
Diwani wa kata ya bugarama Nixson Igoko akizindua Albamu hiyo kumwakilisha Ezekiel Maige mbunge wa jimbo la Msalala aliyepaswa kuwa mgeni rasmi siku hiyo pembeni ni mmoja wa wafanyabiashara wa kijiji cha Bugarama Masuke Shimba aliyewawakilisha wenzake huku akitoa shilingi milioni moja mwingine ni msanii wa nyimbo za injili Happy Shamawele
Wanakwaya wa madhehebu mbalimbali wakiwa katika maeneo ya viwanja vya kanisa la EAGT Bugarama huku wakisubili zamu yao ya kimba
Shamawele akicheza na waimbaji wake
Ndugu na jamaa wa mwimbaji huyo wakifurahiya uzinduzi huo
Wajomba ,mashangazi wakiwa mbele ya jukwaa tayali kwa kuchangia harambee ya uzinduzi huo
Wananchi wakiangalia na kusikiliza kwa makini nyimbo pamoja na michezo mingine iliyoendelea katika viwanja hivyo vya kanisa.
WANANCHI wa kijiji cha Bugarama na vijiji jirani wametakiwa kuliombea amani Taifa la Tanzania katika kipindi hiki kijachao cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba mwaka huu ufanyike katika hali ya amani ili kupata viongozi bora.
Kauli hiyo imetolewa juzi na mwenekiti wa Serikali ya kijiji
cha BugaramaJimmy Kemano katika uzinduzi
wa albamu iitwayo “UTAMALIZAJE” ya nyimbo za Injili iliyoandaliwa na mwimbaji
wa kanisa la EAGT Bugarama Happy Shamawele iliyofanyika katika viwanja vya
kanisa hilo.
Kemano aliwaomba wananchi hao kuendelea kua na mshikamano wa
kuliombea taifa hili ili kuezakupata amani na kusema kuwa kwa sasa taifa lina
michakato mingi sana ambapo aliwakumbusha kuwa kuna kuipigia kura rasimu ya
katiba hivyo waisome waielewe na kuipitisha na kuwataka kujiandikisha kwa wingi
katika daftari la wapiga kura.
“Ndugu wanachi wa kijiji cha Bugarama na makanisa yote mliopo
hapa naomba tuendelee na ushirikiano wa namna hii lakini pia niwaombe tuweze
kufanya maombi sana kuliombee Taifa letu pia tuwaombee wananchi wetu ili
tuwezekupata amani katika kipindi hiki kijacho cha uchaguzi,”alisema mwenyekiti
wa Kijiji Kemano na kuongeza.
“ Ndugu wananchi sasa hivi Taifa hili lina mambo mengi sana
mnayafahamu, kunakuipigia kura rasimu ya katiba inayopendekezwa hivyo niwaombe muisome na kuielewa ili muipitishe wakati
utakapowadia,pili kunauandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura pia
mjitokeze kwa wingi ili baadaye mchague kiongozi bora.
Pia Kemano akizungumzia hali ya waganga wanaopiga ramri
chonganishi katika Kijiji cha Bugarama aliwapongeza wananchi wa kijiji hicho
kutojihusisha na hali hiyo na kuwaomba waendelee kuwapuuza waganga hao kwani hali
hiyo niya uchochezi dhidi ya mauwaji ya walemavu wa ngozi(ALBINO)pamoja mauwaji
ya wazee vikongwe.
Katika uzinduzi wa Albamu hiyo viongozi mbalimbali wa kijiji
hicho pamoja na viongozi wa dini walizindua albamu hiyo kwa kuichangia fedha
kiasi cha shilingi milioni 6.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Jimmy Kemano pembeni ni Diwani wa kata ya Bugarama bw. Nixson Igoko wakiwa meza kuu huku diwani akimwakilisha mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige aliyetoa shilingi laki mbili kweye uzinduzi huo huku mwenyekiti naye akitoa shilingi laki moja na kumi pamoja na diwani huyo kuchangia shilingi elfu hamsini.
0 comments:
Post a Comment