Migodi ya Acacia kutojihusisha kuchangia makundi ya makanisa
Mwenyekiti wa kijiji cha Bugarama Jimmy Kemano akisalimiana na meneja wa mgodo wa bulyanhulu michelle Ash baada ya kuwasili katika ukumbi wa kanisa la AIC Bugarama
Wanakwaya wa AICBugarama wakiimba Shairi lao mbele ya meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu Bulyanhulu Michelle Ash
Meneja Mkuu mgodi huo Michelle Ash akizungumza na waumini wa kanisa la Aic Bugarama katika uzinduzi waCD ya Video itwayo "KIGANJA"
Kikundi cha kwaya ya Neema kutoka kanisa hilo wakimsikiliza kwa makini meneja mkuu wa mgodi huo
Meneja huyo akimshika mkono wa pongezi mmoja wa waimbaji wa kutoka kundi hilo mara baada ya meneja huyo kukata utepe katika CD hiyo kama ishara ya uzinduzi huo
Wakipata vinywaji walivyoandaliwa na wanakwaya hao
Mwenyekiti wa kijiji cha Bugarama Jimmy Kemano alipata fursa ya kuzungumza na waumini wa kanisa hilo katika uzinduzi huo
Michelle Ash Ash akiwasisitiza waamini hao kuwa mgodi hautajihusisha na makundi ya ya kwaya kutoka madhehebu mbalimbali hapanchini Tanzania
Michelle Ash akizindua CD hiyo, katika mashuhuda hao wa kwanza kulia ni dereva wake,wa pili kulia ni mzee wa kanisa hiloSmon Hano Aic Bugarama,pembeni ya meneja huyo ni Mwenyekiti wa kijiji hicho Jimmy Kemano na kushoto kwa meneja huyo ni mwalimu aliyeajiliwa kumfundisha meneja huyolugha ya kiswahili ili iwe njia rahisi ya kuwasiliana na wananchi wanao zunguka mgodi huo.
Michelle Ash akielekezwa na mwalimu wake James Masatu kuikata manila iliyofungwa katika CD ilikufungua kwa usahihi CD hiyo
Mwimbaji wa Neema kwaya kutoka kanisa la AIC Bugarama,Jemima Lekey akijimwaga siku hiyo ya uzinduzi
Meneja huyo Michele Ash akionyesha vazi la kitenge alicho zawadiwa na wanakwaya hao siku ya uzinduzi wa CD yao ya "KIGANJA".
MENEJA mkuu wa mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu
Michelle Ash amesema migodi inayomilikiwa na kampuni ya Acacia hapa nchini
haina utaratibu wa kuchangia makudi ya kwaya katika madhehebu mbalimbali bali
migodi inajikita katika kuchangia huduma kwa jamii.
Hayo ameyasema jana meneja huyo katika sherehe
za uzinduzi wa CD ya Video ya Neema kwaya iliyofanyika katika viwanja vya
kanisa la AIC Bugarama katika kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala wilayani
Kahama mkoani Shinyanga.
Michelle Ash amesema Kampuni hiyo inajikita
zaidi katika kusaidia shughuli mbalimbali kwa wananchi pamoja na kusaidia huduma
za kijamii kama vile ujenzi wa dhahanati kusaidia vikundi vya wajasiliamali
sambamba na kuboresha miundo mbinu za mabarabara maji,elimu na umeme.
Aidha meneja huyo alichangia kiasi cha
shilingi m.100,000 na kusema fedha hiyo haijatolewa na mgodi bali ametoa yeye
binafsi kwa mapenzi mema na kuungwa mkono kiasi cha sh, (500,000 na
meneja wa fedha katika mgodi huo Benedict Busunzu.
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Bugarama Jimmy
Kemano amesema fedha zilizotolewa na meneja huyo ni mchango wake binafsi hiyo
ni kuzidi kudumisha mahusiano wake na wananchi na ambapo naye alichangia kiasi
cha Shilingi 300,000.
Awali akisoma taarifa yao kiongozi wa kwaya
hiyo,Steven John amesema wamezindua CD ya video iitwayo “KIGANJA” lengo la
kumuita meneja huyo ni kufanikisha fedha kiasi cha shilingi
m.31,920,000/=ziwasaidie ununuzi wa vyombo vya music ikiwa ni pamoja na
kukamilisha jengo lao la biashara.
Habari na PAUL
KAYANDA.
0 comments:
Post a Comment