Monday, March 2, 2015

SERIKALI YAOMBWAKUWASIDIA WACHMBAJI WADOGO KAHAMA/MFUKO WA JAMII NSSF YAHIDI KUSHIRIKIANA NA WACHIMBAJI WADOGO/KAMPUNI YAACACIA KUPITIAMGODIWAKE WA DHAHABU BUZWAGI UMELIPA HUNDI YA MILIONI 843,196,808 KWQ HALMASHAURIYA MJI KAMAHUDUMA YA WANANCHI

 PICHA ZA WASHIRIKI KATIKAMKUTANO MKUU KITAIFA ULIOHUSISHA  VIOMGOZINA WADAU WA MACHIMBO MADOGOMADOGO HAPA NCHI ULIOFANYIKAKITAIFA MKOANI SHINYANGAHUSUSANIWILAYA YA KAHAMA (Picha zote na Paul Kayanda. Kahama








 



MFUKO wa taifa wa  jamii NSSF wilayani kahama mkoani shinyanga umepanga kulisaidia shirika lisilo la kiserikali la wachimbaji wadogo  wa madini   “FEMATA” shilingi bilioni 3 katika uendeshaji wa shughuli za uchimbaji madini ndani ya Migodi  yote nchini.

Hayo yamesemwa jana na mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini Bahati kalekwa katika sherehe ya wachimbaji wadogo uliyofanyika wilayani hapa lengo likiwa kujadili namna ya kukiendeleza chama cha Femata.

Kalekwa amesema chama cha femata kilianzishwa  mwaka 1986 kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo hivyo NSSF wameiomba iwasaidie shiringi bilioni 3 katika uendeshaji wa chama hicho ikiwa nipamoja na kutoa elimu kwa   wachimbaji wadogo.

 Kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho Goden Halinga amesema wamejipanga kuwasidia watoto wanaotumikishwa kazi migodini chini ya umri wao  na kuweza kuwasidia kwa  kushirikiana na mashirika mengine ili kuwanusulu watoto hao ikiwa ni pamoja na kuwapeleka shule ili kuwapatia elimu kwa ajili ya maisha yao ya baadae.

Halinga aliongeza kuwa serikali kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato kuweza kuyahimiza makampuni  kujitokeza kuwekeza ili kuweza kuinua kiwango cha uchumi wa nchi pamoja na kuwainua kimaendeleo  wachimbaji wadogo wa madini katika shughuli zao. 

 HABARI NA PILI JITOBA 
KARIBUNI WASOMAJIWANGU KWA HABARI ZA UHAKIKA  PIA UNARUHUSIWAKUTOA MAONIYAKO TUMIA Email yangu kayandap@gmsil.com












MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI BADO NI KITENDAWILI MSALALA
MKUU WA WILAYA YA KAHAMA BENSON MPESYA
 
 
MGODI wa Dhahabu Buzwagi Gold Mine unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya ACCACIA iliyopo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga umekabidhi hundi ya shilingi milioni 843,196,808 kwa Halmashauri ya mji wa huo kama sevis levi fedha ya huduma kwa wananchi.
 
Akikabidhi juzi hundi hiyo kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama Felix Kimaryo Kaimu meneja wa mgodi huo Mtereko Muganda alisema mgodi umelipa shilingi milioni 843,196,808  ya miezi sita fedha ya huduma kwa wananchi iliyopaswa kulipwa tangu mwaka jana 2014kuanzia Julai hadi Desemba.
 
Alisema kama wawekezaji wanatambua jukumu lao la kuhakikisha wanashirikiana na wananchi katika suala la maendeleo na kuahidi kuwa mgodi utakuwa unalipa fedha hizo kila mwaka mara mbili ambapo watatoa fedha hizo mwanzoni mwa mwaka na wmishoni mwa mwaka lengo ni wananchi wauthamini  mgodi huo kwa kusaidia shughuli za maendeleo.
 
Hata hivyo akipokea hundi hundi ya fedha hizo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama Felix Kimaryo alisema fedha hizo watazitumia kuboresha miundombinu mbalimbali katika Halmashauri ya mji ikiwemo ya barabara,maji,Afya na elimu.
 
Awali mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya alisema hata hivyo mgodi wa Dhahabu Buzwagi Gold mine umekuwa mkombozi na msaada mkubwa katika kusaidia shughuli za maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya Kahama mkoani humo kwa kusapoti shughuli mbalimbali za maendeleo.
 
“Mgodi wa Buzwagi unania ya dhati katika suala la maendeleo ya wilaya ya Kahama na tumeshuhudia awali tulikuwa hatuna barabara za rami nab ado umepanga kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwermo huduma za Afya, maji,elimu ambapo kwa sasa wanampango wa kutuwekea taa za barabarani ili kukomesha uhalifu na kuongeza.
 
“Nitahakikisha serikali inashirikiana nao kikamilifu kabla sijaondoka madarakani wawe wametuwekea barabara zetu zote rami na wamepanga kila mwaka kutengeneza kilomea moja kwa kiwango cha rami katika barabara zetu za mji wa Kahama ambapo wataimalizia ya kutoka kwa kituo cha polisi Kahama hadi Redio Kahama kuunganisha na barabara ya mkuu wa wilaya na baadaye barabara ya Azania hadi kupitia msikiti wa mama Farida”,alisema Mpesya.
Mwisho.
 
 
My Blogger Tricks
blogger

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.