Wasanii watakiwa kutetea wauaji ya Albino
Msanii Elic Elias akiwa mbele ya gari |
WASANII
nchini wameombwa kutunga nyimbo ambazo zitasaidia kufikisha ujumbe kwa serikali
ili kuwatetea walemavu wa ngozi ambao kwasasa wanaishi kwa mashaka hapa nchini.
Wito huo umetolewa leo na
mmoja wa wasanii chipukizi Eric
Elias kutoka katika kikundi cha
muungano kinachofanya kazi za sanaa
wilayani Kahama mkoani Shinyanga wakati akizungumza na redio Kahama Fm.
Aidha
msanii huyo chipukizi amesema kuwa kutokana na hali ya sasa si swali kwa watu
wenye ulemavu wa ngozi ALBINO kuishi kwa mashaka sasa ni wakati muafaka wa
wasanii kuwatetea watu hao kwa kutunga nyimbo za kupinga mauaji hayo.
Elias
amesema wasanii walio wengi hapa nchini wanazidi kutunga nyimbo za mapenzi
ambazo hazina tija yoyote kwa wasikilizaji badala ya kutunga nyimbo zinazotoa
elimu zidi ya mauaji ya ALBINO hali ambayo itasaidia kupungua kwa mauaji hayo.
Hata
hivyo amesema kwaupande wake yeye tayali ametunga wimbo wa MATESO unaoelezea
mauaji ya ALBINO na vikongwe ambao umekuwa ni vita kubwa dhidi ya walemavu
ambapo alisambaza kwa vyombo mbalimbali vya Habari ili elimu izidi kutolewa.
Elias
ambaye ni mkazi wa Mwanza aliyeanza kazi za sanaa akiwa darasa la saba
alimejiunga na kikundi cha muungano wilayani hapa kwa lengo la kuielimisha
jamii katika mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.
0 comments:
Post a Comment