jeshi la polisi kahama lazuwia maandamano
Hapa jeshi la Polisisi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga likiwa tayari kukabiliana na wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA pamoja na wananchi watakaojiingiza katika maandamano hayo yaliyokatazwaWafuasi wa chama hicho wakiwa wamebenba mabango yenyeujumbe mbalimbali wa kulitaka Bunge la katiba linaloendelea mjini Dodoma lisitishwe kutokana fedha za walala hoi kuendelea kupigwa
Jeshi la Polisi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga limezuwia maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilayani Humo ambayo yalipangwa kufanyika leo Kupinga kuendelea kwa bunge maalum la Katiba linaloendelea Mjini Dodoma.
Akizungumza na wafuasi wa chama hicho Mkuu wa Kitengo cha usalama Barabarani Wilayani humo Robert Sewando amesema maandamano hayo yahayapo kisheria hivyo amewataka wafuasi wa chama hicho kutawanyika kabla ya jeshi la polisi halijatumia Nguvu kuwatawanya.
Sewando amesema jeshi la Polisi nchini limepiga marufuku, mikutano na maandamano kwa chama hicho kutokana na kuwepo kwa dalili za uvunjifu wa amani hivyo wanapaswa kutii sheria bila Shuruti.
Hata hivyo viongozi watatu wa Chama hicho ambao ni Mwenyekiti wa uhamasishaji na uenezi kanda ya ziwa Juma Protas Ntahimpera, diwani wa Kata ya Nyihogo Amos Sipemba na Diwani wa Viti maalum Kata ya Kahama mjini Winnifrida Mwinula walishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi.
Katika hatua nyingine wakati jeshi la polisi likielekea kuzuia maandamano, Mama mmoja ambaye hakufahamika mara moja aligongwa na Gari la Polisi na kukimbizwa katika hospitari ya Wilaya ya Kahama kwa matibabu.
Nao baadhi ya wanachana na wanaharakati wa chama hicho wamesema kitendo cha Polisi kuwazuia kufanya maandamano ni kutowatendea haki wananachama wa chama hicho kwani mambo yanayoendelea ndani ya bunge la katiba na kufanya ubadhilifu wa fedha za Watanzania.
Kabla ya Kukamatwa kwake mwenyekiti huyo, Protas alisema ‘’maandamano haya ni ya amani na yamefuata sheria ya Kimataifa ambayo tuliamua kuitumia baada ya kukosa kibali kutoka kwa jeshi la Polisi hapa Kahama’’.Alisema Protasi.
Na Paul Kayanda-Kahama
0 comments:
Post a Comment