MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI BADO NI KITENDAWILI MSALALA
MIMBA NA NDOA ZAUTOTONI BADO NI KITENDAWILI MSALALA
IMEELEZWA kuwa tatizo la mimba mashuleni pamoja na ndoa za utotoni katika kata tatu za Lunguya,Bugarama pamoja na Bulyanhulu katika Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga bado ni kitendawili kisichoteguliwa kutokana na viongozi wake kuwakingia kifua watuhumiwa.
Hayo yalisemwa na Afisa
mradi kutoka Shirika lisilokuwa la serikali la CARE INTERNATIONAL,Gega Bujeje
alipoamua kuwashitaki kwa mkuu wa wilaya hiyo,Benson Mpesya viongo walioshindwa
kufuatilia kesi hiyo katika kikao cha zarula kilichojumuisha watendaji na
mratibu elimu kata kilichofanyika ofisini kwa mkuu wa wilaya kilichohusu
kutafuta ufumbuzi juu ya kesi ya mwanafunzi Sikujua Ndalawa (16) wa darasa
la saba katika shule ya msingi Igwamanoni B.
Bujeje alimweleza mkuu huyo wa
Wilaya kuwa viongozi wa ngazi za vitongoji hadi kata pamoja na watendaji wake
wamekwepa majukumu yao nakushindwa kufuatilia kesi ya mwanafunzi huyo
aliyebebeshwa ujauzito mwaka jana na mwanafunzi mwenzake Masanja Julius na
kuwachia jukumu lakufuatilia kesi hiyo wazazi wa binti hali iliyofanya
mtuhumiwa kuachiwa huru na kesi hiyo kuisha kinyemela.
Kutokana na hali hiyo Bujeje
alisema shirika lake linaendesha mradi wa wanaume na wavulana uanolenga kuleta
mabadiliko ya usawa wa kijinsia pamoja nakupinga ndoa za utotoni huku pia
likiwa na lengo la kutoa elimu ya Afya ya uzazi kwa wazazi wanosomesha watoto
wao na limeamua kufika kwake ili aelewe udhaifu huo wa viongozi.
Hata hivyo Bujeje alimueleza
Mpesya kuwa mimba mashuleni pamoja na ndoa za utotoni bado ni changamoto kubwa
katika kata hizo za Halmashauri ya Msalala na alimuomba mkuu wa wilaya hiyo
kuingilia kati hali hiyo ili kuwanusuru wanafunzi wanaokatisha masomo yao na ikiwezekana
afuatiliwe hati ya mashtaka ili achukuliwe hatua kijana huyo aliyeachiliwa huru
huku upo ushahidi wa kutosha.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya
,Benson Mpesya kutokana na hali hiyo aliwaagiza watendaji pamoja na mratibu
elimu kata kuifuatilia upya kesi hiyo ikiwa ni pamoja na kumkamata mtuhumiawa
huyo Masanja Julius(17) ambaye ni mkazi wa igwamanoni ambapo pia aliwaagiza
polisi kufikisha hati hizo za mashtaka ofisini kwake ili ikibainika udhaifu
huokutokea kwa viongozi wake awachukulie hatua za kinidhamu.
Mpesya alisema sheria no.9 ya
ubakaji na sheria no.25 ya elimu inawaruhusu watendaji na waratibu elimu kata
kuchukua hatua kali dhidi ya watuhumiwa hao waliojihusisha na vitndo hivyo
ikiwa ni pamoja na kuwafungulia mashtaka na kuhakikisha wanafuatilia kesi hizo
mpaka mwisho hiyo ni kukwepa majukumu yao pamoja na kutotekeleza shughuli za
Serikali.
Aidha Mpesya aliwataka wazazi
kuepuke kupokea vitu vidogovidogo pamoja na kuwaoza watoto wao wakiwa katika
umri mdogo huku wakiwa bado wanasoma ni kukiuka sheria ambapo pia aliwataka
kuwa na muamko juu ya elimu sambamba na kuwafichua wahalifu pengine kwa
kufikisha malalamiko yao
pale viongozi wao wanaposhindwa kuwasaidia ili kuisaidia serikali.
Mpesya aliwataka wananchi
kushirikiana na Serikali kulipa sapoti shirika hilo ili kuibua maovu yanayoendelea kwenye
jamii hiyo ili kuleta mabadiliko katika usawa wa kijinsia.
NA
PAUL KAYANDA,KAHAMA
0 comments:
Post a Comment