ALIYEFUKUZWA CHADEMA AJIUNGA NA NCCR-MAGEUZI
Makao Mkuu ya NCCR-MAGEUZI
Mbunge wa Kasuru, Moses Machali (katikati) akizungumza kabla ya
kukabidhi kadi ya uanachama kwa mwanachama mpya aliyejiunga na chama
hicho.
Eddo Makata akizungumza na waandishi wa habari baada ya kujiunga na NCCR-MAGEUZI.
jijini Dare ess salaam
BAADA Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
kumtimuwa uwanachama Edo Mwamalala, hatimaye mwanachama huyo ametangaza rasmi
kujiunga na Chama cha Mageuzi ya Taifa (NCCR- Mageuzi).
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo, Mwamalala, alisema harakati za kisiasa alizianza tangu akiwa kijana, kuwa
muumini wa siasa za upinzani na rasmi alijiunga na Chadema.
Alisema ameamua kujiunga na Chama hicho kutokana na
ukweli kwamba ndicho chama kinachoonekana kuwa chama chenye utu, misingi bora
ya usawa, uheshimu wa haki za wanachama na Watanzania pamoja na mshikamano.
“Kwa furaha kubwa kabisa na penda kuchukua fursa hii
kuwatangazia Wanambeya na umma wa Watanzania kwa kuvunja ukimya na sasa
natangaza kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi na nisema kuwa huu ni mwanzo tu
mimi nimetangulia na wengine watakuja au kufuata hatua kwa hatua”alisema
Mwamalala.
Hata hivyo, Mwamalala alipinga kuwa alifukuzwa chama
bali kilichotokea ni kwamba mwanzoni mwa Januari 3 mwaka huu alitangaza
kujiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya Chadema ikiwa ni pamoja na kujivua
uanachama wa chama hicho.
Pamoja na kudai kuwa hajafukuzwa, taarifa za Chama
hicho zinaeleza kuwa Mwamalala alifukuzwa uwanachama tangu mwaka jana

NA PAUL KAYANDA-DAR.
0 comments:
Post a Comment