Tuesday, August 26, 2014

MTOTO ABAKWA KISHA KUTOBOLEWA MACHO HUKO SHINYANGA

Kamanda Justus Kamugisha
Mtoto aitwaye Happiness Kashindye mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Negezi iliyopo kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga ameuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi ambapo mwili wa marehemu ulikutwa kichakani.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dkt Daniel Maguja amesema vipimo vinaonesha kuwa mtoto huyo alibakwa na kutobolewa macho.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  na kuongeza kuwa chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa huku akitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini na kuwakamata wauaji ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Na Kadama Malunde-Shinyanga
My Blogger Tricks
blogger

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.