KKKT KAHAMA YAPANGA KUOKOA VIJANA KWA KUWAJENGEA SEKONDARI YA UFUNDI ILI KUKABILIANA NAAJIRA KWA VIJANA WANOKOMEA KIDATO CHA NNE
CHUNGAJI WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHELI TANZANIADAYOSISIKUSINI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIAJIMBO LAKUSINI MAGHARIBI,DANIEL MONO AKIREKEBISHA ILI ASKOFU WA KANISA HILO EMMANUEL MAKALAmAKALA AKIBARIKI SEHEMU ALIYOWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO LA SHULE YA SEKONDARI AGAPE YA UFUNDI
WOTE WAKIWA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO YA KITUME
MCHUNGAJI HUYO MONO AKIWA KIHUBILI KATIKA VIWANJA VYA SEKONDARI AMBAKO WANATARAJIA KUJENGA SHULE HIYO
WAUMINI WA KANISA HILO WAKISIKILIZA KWA MAKINI SHUGHULI ZA KITUME WAKIWA ENEO LINALOTARAJIA KUJENGWA SEKONDARI
MARA BAADA YA KUHITIMISHA ZOEZI LA KICHUNGAJI KATIKA KUBARIKI ENEO HLIO LA UJENZI
KAHAMA.
KANISA la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria,Jimbo la Kusini Magharibi limeadhimia kukabiliana na
ukosefu wa ajira kwa vijana wanaokomea kidato cha nne kwa kujenga Shule ya
Sekondari ya Ufundi itakayotoa mafunzo ya stadi za maisha.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi;Mchungaji
Daniel Mono katika taarifa aliyoisoma mbele ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Askofu Emmanuel
Makala,wakati wa kuweka Wakfu ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya ‘’Agape’’.
Mchungaji Mono alisema ujenzi wa Shule ya
Sekondari ya Ufundi ‘’Agape’’ itakayojengwa kwa awamu nne utagharimu jumla ya
Shilingi 520,623,740/= ambapo shule hiyo itakuwa msaada mkubwa wa kumudu
kujitegemea kimaisha kwa vijana watakaobahatika kusomea shule hiyo.
Alisema lengo kubwa la kuanzishwa kwa sekondari
hiyo ni kuwapatia wanafunzi masomo ya ziada ya ufundi ambayo ana hakika
yatakuwa mkombozi mkubwa wa kuondokana na maisha ya utegemezi kama walionayo
vijana wengi waliokomea kidato cha nne.
Aidha alisema sekondari hiyo ambayo ni zao la
Agape Primary School,kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo imemudu kufaulisha
kwa darasa zima kwa vijana waliomaliza elimu ya msingi hupoteza mwelekeo wao wa
kitaaluma kutokana na kukabiliana na mazingira mapya yanayowabadirisha
kimaadili kutoka waliyozoea ya Kanisa.
Mchungaji huyo alisema matarajio ya Sekondari
hiyo ni kuanza January 2016,ambapo mbali na kuwajengea vijana stadi za maisha
ili kuondokana na dhana ya kuajiriwa pia itakuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya
Dayosisi kwa kuongeza samani na majengo pindi wanapokuwa katika mafunzo ya
vitendo.
Akifafanua hatua za ukamilishaji wa Sekondari
hiyo,awamu itahusu madarasa manne na ofisi ambayo itagharimu Shilingi 100,623,740/=,awamu
ya pili itakayohusu ujenzi wa ….,jiko na….. na kugharimu Shilingi
150,000,000/=.
Awamu ya tatu itakuwa ni kujenga jengo la
Utawala na Karakana ya ufundi itakayogharimu pia Shilingi 150,000,000/= huku
awamu ya mwisho itakayohusu nyumba za walimu ambazo zitagharimu Shilingi
120,000,000/= hivyo kuwaomba wafadhili na marafiki wa kanisa kujitokeza
kuchangia ili kukamilisha kwa wakati sekondari hiyo.
Nae Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania “KKKT”Jimbo la Kusini Magharibi;Emmanuel Makala aliwaasa
watakaosimamia ujenzi huo kuwa waadirifu na kuhakikisha mradi huo unakuwa na
akaunti yake isiyoingiliana na ya miradi mingine ya Kanisa.
Askofu Makala katika kuhakikisha hilo
linafanyika alianzisha Harambee ya ufunguzi wa akaunti hiyo ambapo zilipatikana
kiasi cha Shilingi Milioni Moja taslimu.
Na Paul Kayanda.
0 comments:
Post a Comment