KDFA CHATAKIWA KUTOINGIZA SIASA KATIKA MPIRA WA MIGUU KAHAMA
PICHA YA JENGO LA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU KDFA(W) KAHAMA LILILOPIGWA KWA NJECHAMA cha mpira wa miguu (KDFA) Wilayani Kahama mkoani Shinyanga kimetakiwa kuacha kuingiza Siasa katika mpira wa miguu na badala yake wajikite katika kuboresha Uwanja wa michezo wa Halmashauri ya Mji wa Kahama pamoja na kutojinadi katika majukwaa ya siasa kwamba ofisi ya michezo imejengwa na Kada wa CCM.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wadau wa michezo Wilayani humo wamemtaja mwenyekiti wa KDFA,Ibrahim Khan kuwa hujinadi katika majukwaa ya siasa kwamba amejenga Ofisi ya michezo katika uwanja wa Halmashauri ya mji huo.
Sambamba na hayo pia Ofisi hiyo imekuwa ikichakaa siku hadi siku ambapo ukiingia kwa ndani milango hakuna wala madilisha pamoja na kukosa vitu ambavyo vinaifanya iitwe Ofisi Hali ambayo inawabidi viongozi wenzake wanapokuwa na shida humfuata ofisini kwake CCM kutokana na yeye ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Wilayani Kahama .
Wadau hao wa michezo wameuomba uongozi wa Halmashauri ya mji huo wasaidie kuitengeneza Ofisi hiyo ili shida ya kimichezo inapotokea wafike katika Ofisi hiyo na si kwenda katika Ofisi za CCM kwani kunaleta shida kubwa katika kuusaka uongozi wa Chama cha mpira wa Miguu tofauti na wilaya zingine au mikoa mikubwa.
Kwa upande wake Afisa utamaduni wa Mji wa Kahama bw, Julius Kambarage alipoulizwa juu ya ujenzi wa Ofisi hiyo amesema kuwa jukumu la kujenga Ofisi ya Chama cha Mpira haihusiani na Halmashauri yake isipokuwa ni jukumu la Chama cha mpira wa miguu wilayani humo, KDFA, Halmashauri jukumu lake nikujenga Uwanja .
Amesema iwapo KDFA inatambua wazi kuwa wadau wake wanahangaika kuwasaka viongozi wa Chama hicho watafute hata sehemu nyingine ya ofisi au waboreshe Ofisi yao pamoja na kuweka walinzi watakaolinda mali za Ofisi hiyo.
Hata hivyo Blog hii ilimsaka mwenyekiti wa KDFA, Ibrahim Khan ambapo alisema kwamba ni kweli pamoja na kujenga Ofisi hiyo Wananchi wasiokuwa na wadilifu wanaiba vifaa vilivyowekwa ndani pamoja na kuiba baadhi ya madirisha na milango hali iliyotulazimu kuziba mlango wa huko nyuma kwakuwa Halmashauri tayari ilikwishaweka mlinzi hivyo bado chama kinajipanga kuiboresha zaidi ofisi hiyo.
0 comments:
Post a Comment