MASHINDANO YA MBIO ZA BASKEL CUP KANDA YAZIWA YATIA FOLA KAHAMA
NKAMIA AKIWA ANAJIANDAA KWA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDINAIBU WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI VIJANA NA MICHEZO, JUMA NKAMIA
HAPA WAKIWA BADO WANAJIANDAA TAYARI KWA MASHINDANO
MICHUANO HIZO ZIKISHIKA KASI ZAIDI
MAENEO YA MWAKATA KUELEKEA SHINYANGA VIJIJINI
KASHESHE LILIKUWA HIVI KUFA NA KUPONA KUWANIA KITITA CHA SILINGI MILIONI MOJA NA LAKI TANO
HILI NDILO GALI LILLOKUWA LIKITOA HUDUMA NDOGONDOGO KWA WASHIRIKI WA MBIO ZA BAISKELI NJIANI
WAPENZI WA NA MASHABIKI WA MBIO ZA BAISKELI WAKIWA WAMEZIZIMA KWA KUFURIKA BARABARA ZA MJI WA KAHAMA
MAMIA YA MASHABIKI MBALIMBALI WA MBIO ZA BAISKELI WAKIWA WAMEFURIKA KATIKA UWANJA WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA
MKUU WA WILAYA YA KAHAMA AKIONGOZANA KUPANDA JUKWAANI NA NAIBU WAZIRI HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO,JUMA NKAMIA KATIKA UWANJA WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA
MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA,JAMES LEMBELI AKIMNONG'ONEZA NAIBU WAZIRI WA HABARI,UTAMADUNI,VIJANA NA MICHEZO,JUMA NKAMIA ALIYEVAA KOFIA
Mashindano ya mbio za
baskel wilayani kahama mkoani shinyanga yazidi
kutimuwa vumbi katika viunga
mbalimbali wilyani humo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji wa Madini
African Barick Gold.Kupitia mgodi wa dhahabu Buzwagi ABG wakishirikiana na
chama cha waendesha Baiskel Tanzania.
Mashindano hayo
yaliyokuwa pata shika nguo kuchanika kutafuta mshingi wa kwanza hadi wa
ishirini kwa wavulana pamoja na wasichana ambapo yalikutanisha mikoa 6 ya kanda
ya ziwa ambayo ni Mara, Mwanza ,
Geita,Kagera, Simiyu pamoja na shinyanga.
Katika mbio hizo za
baskel zilizowakutanisha washiriki wa jinsia zote huku wavulana wakikimbia
kilometa 156.5 kutoka maeneo ya fantom kuelekea manzeshe hadi shinyanga
vijijini ambapo wasichana wakikimbia kilometa 80 kutoka maeneo ya fantom
kuelekea manzese hadi Sungamile Isaka,huku wote kumalizia mashindano hayo
katika barabara ya Bijampola mjini
kahama.
Kwaupande wake katibu
Mkuu Taifa chama cha waendasha baskel
John Machemba awali akizungumza katika ufunguzi wa mbio hizo wilAyani humo
amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kutafuta washindi 20 kutoka pande zote
mbili kwa wanaume pamoja na wanawake ili kwenda kushiriki katika shindano
lililoandaliwa huko mbeya litakalo shirikisha kanda 6.
Machemba alimtanganza
mshindi wa kwanza kuwa Masunga Duba kutoka mwanza aliyekimbia
masaa 4 na sekunde 3 huku akipata zawadi ya shillingi million 1.5, Medali
pamoja na kikombe huku mshindi wa pili akitajwa kuwa ni Seni Konda kutoka
shinyanga huku akipatia Tsh.million 1 na Medali pamoja na Kikombe.Pamoja na
mshindi wa 3 Simon Mbaluku kutoka simiyu akipatiwa Tsh,laki 7.
Huku Mshindi wa 4
hadi wa 10 walipatiwa Tsh.laki 2.5 pamoja na wengine waliobaki ambao
hawakuingia katika kumi bola walipatiwa Tsh,laki 1.5 ili kuwahamasisha
kushiriki katika mashindano mengine kwa mwaka ujao.
Kwaupande wake Makamu
wa Rais wa Kampuni ya uchimbaji Madini African Barick Gold.Kupitia mgodi wa
dhahabu Buzwagi ABG,,Deo Mwanyika amesema kuwa kampuni hiyo inawajali wananchi
huku lengo lake ikiwa ni kukuza vipaji mbalimbali ya vijana huku akiwataka
kutumia fursa hiyo ili kutambua uwepo wawawekezaji katika maeneo yao
Nae naibu waziri wa
habari,utamaduni vijana na michezo Juma Nkamia ameitaka halmashauri ya mji wa kahama kutumia fursa
hiyo ya wawekezaji kukuza vipaji mbalimbali ya vijana ikiwa ni pamoja na
kubolesha mazingira ya michezo hususani uwanja
wa michezo wa halmashauri hiyo.
Pia ameutaka uongozi
wa mgodi huo kushirikiana na ofisi yake katika kuulekebisha uwanja wa michezo
wa halmashauri hiyo huku mgodi ukibolesha uzio(UKUTA) na ofisi yake
ikipandikiza majani ya bandia pamoja na kubolesha mazingira ndani ya uwanja
huo.
Na Paul
Kayanda, Kahama,
0 comments:
Post a Comment