KESI YA WAUMINI DHIDI YA ASKOFU WAO YAANZA KUSIKILIZWA SHINYANGA
Waumini wa kanisa la EAGT Majengo mjini Shinyanga wakiwa katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga wakiwa wameshikilia mabango
Kesi inayomkabili Askofu wa Kanisa la (EAGT) , kanda ya Magharibi Rafaeli Machimu,Dhidi ya waumini wa dhehebu hilo lililopo Majengo Mjini Shinyanga ,kwa madai ya kuwanyanyasa kwa kumfukuza Mchungaji wao David Mabushi bila kosa lolote ambaye bado wanamuhitaji imeanza kusikilizwa mahakamani.
Kesi hiyo imeanza kusikilizwa jana katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga,lakini mahakama imeahirisha shauri la kesi hiyo, lililofunguliwa na waumini baada kuona upande wa mlalamikaji haukukidhi vigezo vya sababu ya kufungua shauri hilo.
Akisoma shauri ya kesi hiyo hakimu mwandamizi wa wilaya Thomson Mtani katika mahakama hiyo alisema mahakama imeona kwa upande wa mlalamikaji kuwa shauri dogo namba 08/2014 lililofunguliwa kupitia kwa mwanasheria Norbat Beda halina sababu ya kufunguliwa kwake.
Hakimu Mtani alimuomba wakili wa upande wa mlalamikaji Norbat Beda aandike upya sababu za msingi za kufungua kesi hiyo, ili wakili wa upande wa pili wa mlalamikiwa Bartazar Mwairo aweze kujibu haraka shtaka hilo dhidi ya mteja wake siku ya kesi iliyopangwa kusikilizwa tena Agoust 28 mwaka huu.
Shauri hilo lililokuwa linapinga kitendo cha Askofu wa kanisa la EAGT kanda ya Magharibi kumwandikia barua ya kumfukuza mchungaji Mabushi katika kanisa hilo itasomwa tena agosti 28 mwaka huu
Aidha kesi hiyo ilianza kutajwa tarehe 4 Agosti ,2014, katika mahakama ya wilaya na mara ya pili ilisikilizwa Agosti 14, na kuahirishwa kusikilizwa kwa sababu wakili wa mshitakiwa aliiomba mahakama iahirishe kusikilizwa kutokana na kutoelewa kina cha kesi hiyo hivyo ilitarajiwa kusikilizwa tena Agosti 25 imeahirishwa tena mpaka Agosti 28 mwaka huu.
Waumini wa kanisa hilo walimfikisha mahakamani Askofu Rafael Machimu Agost 4 mwaka huu, kwa madai ya kuwanyanyasa kwa kuwafukuza mara kwa mara wachungaji wa kanisa lao la( EAGT),la Majengo Mjini Shinyanga bila ya Sababu za msingi.
Walisema kanisa hilo lilianzishwa mwaka 1992 likiwa chini ya mchungaji John Chambi ambaye aliondolewa na uongozi wa jimbo la Shinyanga akiwepo mchungaji Rafael Machimu ambaye wakati huo alikuwa katibu wa jimbo hilo.
Waumini hao walisema tangu mwaka huo waliendelea kuabudu bila mchungaji hadi mwaka 1999 kanisa hilo lilipelekewa mchungaji Mothes Kuzenza ambaye kwa sasa ni marehemu naye aliondolewa mwaka 2003 katika mazingira ya kutatanisha.
Walisema walivyofuatilia waligundua kuwa ameondolewa kupitia mkono wa Askofu Rafael Machimu ambaye wakati huo alikuwa katibu wa kanda, na kudai wamechoka kuona wachungaji wao wakiondolewa mara kwa mara bila ya makosa.
“Kwa kweli tumechoka kuondolewa ondolewa wachungaji mara kwa mara tumeamua sasa kwenda katika ngazi ya mahakama tuone kama mchungaji wetu Mabushi kama atakuwa na makosa ya kuondolewa katika kanisa la majengo,”.
“Sisi ndiyo waumini wa hili kanisa na ni waumini wa miaka mingi hakuna mali ya EAGT hata bati moja haijaleta, mali iliyopo humo ni mali ya waumini na hatu taki kunyanyaswa bado tunamhija mchungaji wetu David Mabushi”,walisema waumini hao.
0 comments:
Post a Comment