Wednesday, March 5, 2014

CHINJACHINJA YAINGIA TENA KAHAMA

Mtoto Said Sirajiakiwa na bibi yake mzaa mama Ashura Ngasa na Mama yake mdogo Maimuna Idd ambao wanamuuguza
Dakta Fwoma amesema baada ya kufikishwa hospitalini madaktari walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo aliyochinjwa na hadi alasiri hii hali yake imeendelea vizuri hasa baada ya kuongezwa damu.




Kwa mujibu wa mama mzazi wa Siraji Mariamu Idd(35) amesema, Mtoto Siraji jana alichukuliwa na baba yake mzazi anayeitwa Siraji Salvatory(45) kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa wazazi hao walikwishaachana siku nyingi.

Leo asubuhi Mariam amepigiwa simu akielezwa taarifa za kuchinjwa kwa mwanae na baba yake mzazi, ambaye baada ya tukio hilo amekimbilia kituo cha polisi Mjini Kahama kwa lengo lakujisalimisha na kwamba hadi sasa ameshikiliwa huko.

Mariam amesema, awali Salvatory alikuwa akimchukua Siraji mara kwa mara na kumpeleka nyumbani kwake Malunga na baadaye kumrudisha akidai kuchoshwa na huduma za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya kiafya.

Jeshi la Polisi wilayani Kahakama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa linaendelea na upelelezi na kwamba baada ya kukamilisha litamfikisha mahakamani Salvatory kujibu tuhuma zinazomkabili.
My Blogger Tricks
blogger

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.