Thursday, February 6, 2014

WANA CCM KAHAMA WACHARANGWA MAPANGA WAKITOKA KWENYE KAMPENI

KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Kahama;Masoud Melimeli {34}ambaye ni miongoni mwa majeruhi waliokatwa mapanga na watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa CHADEMA.

MWANDISHI wa Habari wa gazeti la Mwananchi mkoani Shinyanga;Shija Felician akingalia sehemu ya majeraha aliyoyapata Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kahama;Masoud Melimeli aliyoyapata baada ya kushambuliwa na wafuasi wanaodaiwa wa CHADEMA walipokuwa wakitoka katika mkutano wa kampeni wa Uchaguzi mdogo katika kata ya Ubagwe.

 MMOJA wa vijana wa CCM;Ramadhani Salumu [25]mkazi wa Mwendakulima wilayani Kahama ambaye pia alijeruhiwa na mapanga katika kadhia hiyo.

 AFISA Mtendaji wa Kata ya Ubagwe;Alphonce Kimaro ambaye naye alijeruhiwa akiwa amepatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kabla hajahamishiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando.

MWENYEKITI Mstaafu wa CCM wilaya ya Kahama;Andrew Masanje akimjulia hali katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Kahama;Masoud Melimeli.


 DREVA wa gari la CCM wilaya ya Kahama;Charles Peter [55] akiwa katika hospitali ya Halmashauri ya Kahama kabla hajahamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando.




MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Kahama;Machibya Jiduramabambasi katikati akimuangalia Afisa Mtendaji wa Kata ya Ubagwe;Alphonce Kimaro {50} aliyecharangwa mapanga kichwani wakati wa kampeni za Udiwani katika Uchaguzi Mdogo wilayani Kahama,nyuma yake ni Muuuguzi Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama;Richard Mabagala.
 AFISA Mtendaji wa Kata ya Ubagwe;Alphonce Kimaro akiwa wodi ya majeruhi ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kabla hajahamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.
WAFUASI sita wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Kahama wamelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kucharangwa mapanga kwenye kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Ubagwe.
 
Kwa mujibu wa Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama;Richard Mabagala amesema katika vurugu hizo zimemjeruhi Afisa Mtendaji wa kata hiyo Alphonce Kimaro ambaye amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa mapanga kichwani.
 
Muuguzi Mkuu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama;Richard Mabagala amewataja wengine waliojeruhiwa kwa mapanga na kulazwa hospitalini hapo ni pamoja na Sebastian Masunga {34].
 
Aidha Mabagala amewataja wengine ni pamoja na Ramadhani Salumu,Subira Nyangusu  na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kahama;Masuod Melimeli{34} pamoja na dreva wa gari la CCM wilaya;Charles Peter {55} .
 
Hata hivyo Mganga Mkuu wa wilaya ya Kahama;Andrew Emanuel amesema Kimaro,Masunga na Peter hali zao ni mbaya wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Habari za polisi zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga;Evarist Mangala tayari watuhumiwa 16 wa tukio hilo wamekamatwa akiwemo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki;Sylvester Kasulumbayi wote wakiwa wafuasi wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
My Blogger Tricks
blogger

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.