HUHESO FOUNDATION YAMPATIA VIFAA VYA SHULE MWANAFUNZI MMOJA WA SEKONDARI YA NYASHIMBI KAHAMA
JUMA MWESIGWA AKIKABIDHI VIFAA MBALIMBALI KWA MWANAFUNZI YUSUPHU LAZARO MBELE YA WANAFUNZI WENZAKE PAMOJA NA WALIMU WAKE.WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYASHIMBI WAKIWA KATIKA MABADILISHANO YA MAWAZO KWAMBA NIJINSI GANI KATIKA KUELIMISHANA KUHUSU ELIMU
KAIMU HUYO BW.PELIUS AKIWA ANALISHUKURU SHIRIKA HILO
JUMA MWESIGWA NA WANAFUNZI
MWESIGWA AKIWA ANAMKABIDHI VITABU VYA SHERIA YA HAKI ZA WATOTO MBLELE YA WANAFUNZI WENZAKE
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYASHIMBI WA KIDATO CHA PILI WAKIWA NDANI YA DARASA LAO
KAIMU MKUUWA SHULE HIYO BW.PELIUS AKISALIMIANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA HILO JUMA MWESIGWA KATIKA UKUMBI WA DARASA
YUSUPH LAZARO (17) AKIWA NA VIFAA VYA SHULE ALIVYO PATIWA NA SHIRIKA LA HUHESO FOUNDATION
KAIMU MKUU WA SHULE YA SEKONDARI NYASHIMBI BW.CELESTIN PELIUS AKIWA KATIKA DARASA LA KIDATO CHA PILI
WAKIWASILISHA KAZI ZAO KWA MWALIMU WA SOMO
WAKIJIPANGA FOLENI KWENDA KUSAHIHISHWA KAZI ZAO ZA KILA SIKU
WKIWA WAMEPAKI USAFIRIWAO HUKU WAKIENDELEA NA MASOMO YAO
WANAFUNZI WASHULE YA SEKONDARI NYASHIMBI WAKIWA KATIKA ENEO LAO LA SHULE
SHIRIKA la HUHESO FOUNDATION lenye makao makuu yake katika kata ya Malunga
Wilayani Kahama mkoani Shinyanga limempatia mwanafunzi mmoja Yusuph
Lazaro(17)wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Nyashimbi vifaa mbalimbali
ikiwa ni seti ya madaftari kalamu pamoja
na fedha taslim sh.60,000 ya michango mbalimbali.
Akikabidhi
viaa hivyo shuleni hapo mkurugenzi
wa shirika la HUHESO FOUNDATION;Juma Mwesigwa alisema kuwa Lazaro alifika katika ofisi za HUHESO kwa lengo la kuomba msaada wa vifaa
mbalimbali vitakavyomsaidia kimasomo
ambapo alifafanua kuwa kutokana na shirika lake lianajikita zaidi
kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hasa mitaani na mashuleni
nakuongeza kuwa shirika lake lilifanya jitihada za kumsaidia mwanafunzi huyo
kutoka kwa wadau mbalimbali kupitia katika mitandao ya kijamii.
Alisema kutokana na hali hiyo wadau wengi walioguswa
waliweza kutoa michango mbalimbali ya fedha, madaftari pamoja kalamu na vitu
vingine vya masomo.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa shule hiyo;Celestin
Pelius akilishukuru shirika hilo alisema kuwa
ni mashirika machache yanayo weza kwenda moja kwa moja kutoa misaada
hiyo bila kupitia serikalini hali iliyomfurahisha mkuu huyo.
Alisema
misaada mingi inayotolewa na mashirika binafsi haiwafikii walengwa kwa
wakati na badala yake huishia katika mikono ya watu wachache na mwisho wa siku
wanabaki kuilaani serikali kuwa haiwabani wanaohusika.
Kwa upande wao walimu washule hiyo kwa pamoja
wakiushukuru uongozi wa shirika hilo kwa kuliona suala hilo katika shule yao
walisema kuwa shirika lizidi kusaidia katika shule hiyo ambapo walisema licha
ya lazaro kuna wengine wengi katika shule hiyo
wanaohitaji kusaidiwa.
Kwa upande wake Yusuph Lazaro akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa
analishukuru shirika hilo kwa kumlipia ada ya shule pamoja na vitu mbalimbali
vya masomo ambapo aliongeza kuwa shirika liendelee kuwajali hasa watoto waishio
katika mazingira magumu na wenyenia ya Elimu.
0 comments:
Post a Comment