MWANZIRISHI wa vikundi mbalimbali katika kata ya kinaga wilayani Kahama katia mkoa wa ShinyangaEmmanuel Magoso ambae pia ni mkurugenzi wa vikundi hivyo Akimraki mh. Diwani wa kata hiyo Mary Manyambo alipokuwa akihudhulia hafla hiyo fupi ya kutoa misada hiyo kwa watoto hao.
WATOTO wa shule mbalimbali za msingi katika kata ya Kinaga wakiwa tayari kwa kupokea misaada hiyo.
MH>DIWANI kata ya Kinaga akiendelea na zoezi zima la ugawaji wa misaada kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la saba pamoja na watoto wasio soma wakiwemo wazee wasiojiweza.
DIWANI WA KATA ya kinaga Akimkabidhi msaada wa godoro neti na shuka mmoja wa wazee wasiojiweza ambaye pia ni mlemavu wa macho bw.Mathias Luhenzagula.
VIONGOZI WA kikundi cha TUMAINI NDUKU CENTRE wkijadili kwa kunog'ona mbele ya umati wa wtu waliohudhulia katika hafla hiyo.
MKURUGENZI wa vikundi vya wajasilia mali katika kata ya Kinaga EMMANUEL MAGOSSO ambaye pia ni mwanzilishi na mshawishi katika vikundi hivyo vya wajasilia mali katika kata hiyo wilayani humo, akiwa anaweka mambo sawa katika computer yake ya mkononi
BAADHI ya watoto waishio katika mazingira hatarishi zaidi kiiji cha Nduku katika kata ya Kinaga kilichopo katika halmashauri ya mji wa Kahama.
MWENYEKITI wa kikundi cha TUMAINI NDUKU CENTRE akiwa antoa nasaha zake mbele ya diwani wa kata hiyo.
MWENYEKITI msaidizi wa kikundi cha TUMAINI NDUKU CENTRE katika kata ya kinaga DOTTO MARANDO akitafakari jinsi ya kuendesha kikundicho.
MWENYEKITI wa kikundi cha Tumaini Nduku Centre akipongezwa na diwani wa kata ya Kinaga Mary Manyambo kwa hatua aliyoifikia hadi kutoa misaada hiyo kwa waoto waishio katika mazingira hatarishi zaid i pomoja na wazee wasiojiweza kimaisha.
Na Paul Kayanda,
Kahama
November,3,2013
KAHAMA
IMEELEZWA kuwa zaidi
ya watoto 78 waishio katika mazingira
Hatarishi zaidi katika kijiji cha
Nduku katika kata ya Kinaga Wilayani Kahama Mkoani Shinysnga Wamepatiwa msaada wa vifaa mbalimbali pamoja na nguo za
shule,kalamu,daftari, mafuta ya kupakaa,godoro pamoja na shuka vikiwa na
thamani ya sh. Laki tano.
Hayo yameelezwa jana
na katibu msaidizi wa kikundi cha Tumaini centre; Nzile Lukondya, katika hafra fupi ya kugawa misada hiyo iliyofanyika katika
kijiji cha Nduku wilayani humo,wakati
akisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi diwani wa kata ya Kinaga Mary Manyambo, akimwakilisha mkurugenzi wa mji wa kahama, Felix Kimaryo ambapo Lukondya amefafanua kuwa katika utafiti uliofanywa na
Kikundi hicho kilibaini kuwa zidi ya
watoto 78 wenye hali duni zaidi
wanahitaji kusaidiwa.
Ameongeza kuwa kwa kutambua hali hiyo kikundi hicho kimeona
nivyema kitoe mchango huo na kwa hatua
ya kwanza kimeanza kuhudumia watoto 15 ambapo wanafunzi 6kuanzia darasa la
kwanza hadi la saba,mjane 1,watoto wasiosoma 6na wazee2 wasiojiweza,kwa kugawa
nguo za shule,kalamu ,daftari ,sabuni ,mafuta ya kupakaa,godoro,masheti pamoja
na suluali.
Akikabidhi misaada hiyo Diwani wa kata ya Kinaga bi.Mary Manyambo alianza kwa
kumshukuru mwanzilishi wa vikundi vya wajasiliamali wa kata ya Kinaga; Emmanuel
Magoso kwa ushawishi wake katika kuanzisha vikundi hivyo ambapo alikipongeza
kikundi hicho kwa kufanikiwa
katika hatua hiyo,pamoja na kuwashukuru viongozi hao kwa maazimio ya
kulenga kupunguza nakulikabili wimbi la watoto nawaze wasiojiweza kuwa
ni tatizo na kero kubwa katika jamii.
Aidha
bi. Manyambo ameongeza kuwa kwa sababu hiyo kunahaja ya vikundi vingine
kuongezeka ili kukabiliana na janga hilo,ambapo manyambo ameeleza
kuwa serikali bado inachangamoto kubwa ya kuhakikisha inapambana na
janga hilo kwa kushirikiana na vikundi pamoja taasisi zauma na
mashirika mbalimbali ya hapa nchini.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kikundi hicho ;Mussa Mayala kipindi cha
tarehe 27januari mwaka huu kikundi chake kiliunda uongozi ambapo
alichaguliwa mwenyekiti Mussa mayala katibu mkuu akiwa Manyanda Ntobela
na kwamba wanakikundi waliweka utaratibu wa kukopa na kutoa hisa
kwaajili ya kutunisha mfuko wa kikundi, wanakikundi hao waliweza
kuchanga kiasi cha fedha shilingi m. 128,000,ambapo fedha hiyo
ilishakwishaanza kukopeshwa.
Hata
hivyo bw. Mayala ameongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo mbele yao ni
kuhakikisha kikundi hicho kinalenga kusaidia vijana, wanawake pamoja na
wanaume ili waweze kujipatia maisha yao wenyewe sambamba na kujitegemea
na kwamba jamii itawaheshimu badala ya kuwadharau.
Mmoja
wa wazee hao wasiojiweza Mathias Luhenzagula akiushukuru uongozi huo
kwa niaba ya wenzake alisema kuwa amefarijika kutokana na kupatiwa
msaada huo wa godoro, neti na shuka, kwakuwa toka azaliwe hakubahatika
kulalia godoro hivyo sasa nimara yake ya kwanza ambapo alimshukuru mora
kikundi hicho kwa kumuona na kupatia msaada huo.
Pia
Luhenzagula ambaye pia ni mlemavu wa macho aliutaka uongozi huo
kuepukana na migongano isiyokuwa ya lazima baina yao na badala yake
wajikite zaidi katika kutoa huduma hizo kwa jamii.
0 comments:
Post a Comment