Thursday, November 21, 2013

Thursday, November 21, 2013

SERIKALI YATAKIWA KUTAMBUA SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

 MKUU WA Wilaya ya Kahama Benson Mpesya  wa kwanza kulia akiwa sambamba na mkurugenzi wa HUHESO foundation wa kwanza kushoto  katika sherehe ya kuwapongeza wasichana 24 waliomaliza mafunzo ya cherehani mjini Kahama ambapo mkuu huyo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo lakini kutokana na majukumu ya kikazi hakumudu sherehe hiyo na badala yake aliweka mwakilishi.


 MKURUGENZI wa HUHESO Juma Mwesigwa akisoma majina ya wasichana hao ili kukabidhiwa cherehani zao  na mgeni rasmi aliyemwakilisha mkuu wa Wilaya hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa msalala bw.Patrick Karangwa Charles alikabidhi cherehani hizo kwa wasichana wote 24 ambao walipata mafunzo hayo ndani ya miezi mitatu.
 BW. Patrick Karangwa Charles akikabidhi cherehani kwa wahitimu wa mafunzo hayo nje ya ukumbi wa wauguzi PHN  mjini Kahama
 MMOJA WA wasichana katika kundi la wafanya biashara za ngono mjini kahama akiwa na furaha kubwa ya kuhitimu mafunzo hayo pamoja na kupatiwa cherehani na shirika hilo
 WANAHABARI watoto wa shirika la HUHESO FOUNDATION wakiwa makini katika kusikiliza machache katika hafla hiyo  fupi
 HAWANDIYO  wasichana wanaofanya biashara ya ngono katika mji wa Kahama ambao wamepatiwa mafunzo ya cherehani na shirika lisilokuwa la serikali la HUHESO FOUNDATION lenye maskani yake katika kata ya Malunga mjini Kahama ambapo limewapatia cherehani kila mmoja aliyefuzu mafunzo hayo.
 WANANZENGO walioalikwa katika hafla hiyo wakiwa mashuhuda wakubwa katika zoezi la  ugawaji wa vyerehani.
 HAWA NDIYO walimu wa mafunzo hayo kwa wasichana hao ni walimu waliobobea  na mitindo mbalimbali katika fani ya chrehani pamoja na ubunifu na masomo ya ujasilia mali wilayani humo.
 WAHITIMU HAWA wakijaribu kutoa igizo la biashara yao ya awali ya ngono jinsi walivyokuwa na uwezo mkubwa wa kumteka mwanaume na kutoa kiwango kikubwa cha pesa , hali waliyosema kuwa katika kiwango hicho kikubwa cha pesa ni hatari sana na hivyo fursa ya mafunzo hayo  wataitumia kupata kipato chao halali katika shughuli za ushonaji pamoja na ujasilia mali ambapo watakuwa wameepuka biashara hiyo haramu ya ngono ambayo ingewasababishia  maradhi ikiwa nipamoja na UKIMWI.
MKURUGENZI wa MSALALA bw.Charles akiwaasa wasichana hao aliwataka kuepukana na vikundi ambavyo  vinakazi ya kuwapotosha mabinti  wengine na badala yake wawe walimu wakubwa katika jamii kuhusiana na biashara ya ngono,

Aliongeza kuwa  chrehani walizopatiwa  wazitumie kwa kutafuta riziki zoao katika maisha ya kila siku  pamoja  nakuzifanyia mantanesi za mara kwa mara  na kusisitiza mkurugenzi wa huheso kuwatembela marakwamara  ili kubaini mazuri wanayoyatekeleza wahitimu hao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika hilo Juma Mwesigwa aliahidi kuwatembelea mpaka ahakikishe wananufaika na cherehani walizozipata kutoka kwenye shirika lake ambopo pia alisema kuwa atakuwa pamoja na kuwa wamehitimu bado ataendelea kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali za shirika lake nahivyo ameiomba serikali izidi kuunga mkono juhudi  kwa  mashirika  yasiyokuwa ya serikali katika kupambana na majanga yanayoikabili jamii.

Hata hivyo katika kuunga mkono juhudi zinazofanya na mashirika hayo Mkurugenzi  wa Msalala  bw.Karangwa,aliliunga mkono shirika la HUHESO kwa kiasi cha sh. 1,000,000,/= tasilim kwa muendelezo wa  jengo la darasa moja lililo komea njiani kwa ujenzi.

No comments:

Post a Comment

My Blogger Tricks
blogger

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.