RED'S MISS SHINYANGA YAZIDI KUPAMBA MOTO KAHAMA
Huu ni Ukumbi wa chakula uanojulikana kama Nyerere Restaurant (Ihesa Hotel)Nyumba ya kulala wageni Ihesa hotel ambapo warembo hao wameweka kambi
Warembo wanaotarajia kua Miss Shinyanga wakiwa wameketi kwa uzuri kabisa
Warembo wanaowania Reds Miss Shinyanga wakiwa katika mazoezi ya Maonyesho katika viwanja vya Ihesa Hotel
TUNAJIADAI KILA MTU NI MZURI
Warembo hao wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa shindano hilo pamoja na Afisa Utamaduni wa Mji wa Kahama Julius Kambarage wa nne kutoka kushoto
TUMEPENDEZA
TUMEPIGA PICHA NA WAREMBO
Mkurugenzi wa Asela Promotion Asela Aloyce Magaka akiwa katika picha ya pamoja na Afisa utamaduni wa Mji pamoja na wadhamini wake wakwanza kushoto
TUTAKULA CHAKULA
TUNALALA SEHEM NZURI
UMEKA VIZURI
TMEKA NA WAREMBO
TUNAFAA NA TUTASHINDA WOTE
TUMESIMAMA NA MTU MKUBWA
TUPOSAWA
KAMBARAGE AKIWA NA WAREMBO KATIKA PICHA YA PAMOJA
MDHAMINI WA TSMM DUKA KUBWA AKIWA NAWAREMBO KATIKA PICHA YA PAMOJA
MWAKILISHI KUTOKA BUZWAGI MDHAMINI MKUBWA AKIWAKATIKA PICHA YA PAMOJA
TUMEKAA VIZURI
TUNAFANYA MAZOEZI
WADHAMINI MBALIMBALI WA SHINDANO HILO WAKIBADILISHANA MAWAZO NA WANDISHI WA HABARI WAKIWA KATIKA VIWANJA VYA IHESA HOTEL
ZAIDI
ya Warimbwende 20 wanagombea Taji la Kumsaka Mrembo atakayevaa Taji la Miss
Shinyanga 2014 Juni,28 mwaka huu limeandaliwa na Kampuni ya Asela
Promotion chini ya Wadhamini wake 22.
Mkurugenzi
wa Kampuni hiyo Asela Aloyce Magaka akiongea katika ufunguzi wa shindano hilo lililojumuisha
Wadhamini 22 wa shindano hilo Pamoja na Wadau wengine lililofanyika
katika ukumbi wa Ihesa Hotel alisema anatarajia kumpata mrembo makini
atakayelivaa Taji hilo.
Kutokana
na hali hiyo Magaka alisema amekuwa na uzoefu wa kuandaa mataji mengi toka mwaka
1999 pia alidai kuwa uzoefu huo unatokana na yeye kuwa miss Temeke miaka ya
nyuma ambapo alisema ameamua kujitosa katika kuwaendeleza wasichana kwa kuibua vipaji vyao.
Mkurugenzi
huyo alisema Warembo hao watakaoshiriki kinyang’anyilo hicho ni Warembo kutoka
Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Shinyanga ambapo alidai kuwa Washindi
watajinyakulia zawadi kemkem.
Pia
aliwataka warembo hao kujiamini wakati wote kipindi ambacho wapo katika mazoezi
yao nakuwaondolea wasiwasi kwa kuwaeleza kuwa vigezo vya kushinda si uzuri wa
mshiriki bali ni sifa ya kwamba mshiriki anatakiwa aweze kusimama kama Balozi.
Katika
hatua nyingine Mdhamini mwingine Tricie Social Media Market TSMM SYSTEM (DUKA KUBWA) alimwahidi
Mkurugenzi wa Kampuni ya Asela Promotion kuwa atatoa ajira ya mwaka mzima yenye
mshahara usiopungua raki tatu kwa mwezi kwa mrembo atakayeshinda taji hilo.
Awali
akifungua shindano hilo Afisa Utamaduni wa Mji wa Kahama ,Julius Kambarage
amemtaka Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Asela Promotion kuandaa mapema zawadi za washindi na siyo kutegemea pesa zinazokusanywa mlangoni.
Kambarage
amesema kuwa tabia kama hizo zimekuwazikijitokeza katika mashindano mbalimbali ya Warembo hususani Wilayani Kahama.
Amesema Serikali imekuwa ikipokea malalamikao mengi ya kudhurumiwa warembo hao na kusisitiza kuwa kwa sasa hayupo tayari kupokea malalamiko yoyote kuhusu kudhurumiwa kwa warembo hao badala yake yupo tayari kwa kuhakikisha wanapata haki yao.
Amewataka waandaaji wa mashindano inchini wahakikishe wanasaini mikataba na Warembo kabla ya kuanza kinyang'anyilo hicho ili iwe njia rahisi ya kuwabana waandaaji wa mashindano hayo kipindi watakaposhindwa kutoa haki za Warembo hao.
Kambarage amemtaka Mkurugenzi huyo kutangaza mapema Zawadi watakazozitoa ili Mshiriki aridhie kabla ya kusaini mkataba.
Hata hivyo Magaka amesema licha ya Duka kubwa kutoa zawadi ya Mshindi wa Red's Miss Shinyanga pia zawadi itakayotolewa ni kwa mshindi huyo atapata laptop yenyethamai ya sh.700,000 na pesa Taslim sh.500,000.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment