Na Paul Kayanda
Kahama
October,2,2013
AMBURUZA MAHAKAMANI KWA KUTISHIWA KUMWAGIWA TINDIKALI KAHAMA
Aliyekuwa
mtumishi wa jeshi la Polisi katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ;Hassani Maazige “Foma” (38),
Amemfungulia kesi ya kuua kwa tindikali
raia wa Burundi bw.Ahmed Isumail
ambaye ni ndugu na jambazi
aliyewahi kufanya uhalifu sehemu nyingi ikiwa ni pamoja na Kahama aitwae “Gobos” aliyefahamika kwa jina moja.
Awali
akisomewa shitaka hilo linalomkabili September,30,mwaka huu, Bw. Ahmed Isumail ambaye ni Raia wa Burundi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo; H.s. Byalugaba, licha ya kesi yake ya
jinai mshitakiwa huyo alikana
tuhuma zote za kutishia kumwagia
tindikali Bw. Mazige na kutishia kumwua na
silaha kali.
Hata hivyo kesi hiyo ilpangwa tarehe 8 october,2013, kutokana na ukusayaji wa ushahidi ambao utamkabili Ahmedi Isumail kwa tuhuma
ambazo zinasadikika amezirithi
kutoka kwa ndugu yake ambaye ni
Gobosi aliyekuwa jambazi kwa miaka ya nyuma kwa uhalifu.
Aidha bw. Mazige
Akimtuhumu bw.Isumail kwa makosa mbalimbali ya matusi na kumtishia mauaji katika Hotel ya Muleba Bar. Kwa kashifa
za aina nyingi kwa muda mrefu hali
ambayo ilisababisha bw.Mazige kuchukua
uamuzi wa kumfungulia mashitaka ya aina nne kutishia kuua kwa siraha
,kumwagia tindikali,matusi ya nguoni na kashifa mbalimbali ambazo hastaili kuwa
nazo na si haki kumfanyia mtu.
Kwa upande wake hakimu wa mahakama ya mwanzo katika Wilaya ya
Kahama Mh. H.S. Byalugaba aliahilisha kesi hiyo na kuipanga tarehe 8-10-2013 maka huu kwa kuisoma
tena mara ya pili wakati ushahidi
utakapoletwa na Mazige kwa mwendelezo wa kesi yake.
MWISHO
Click here to Reply or Forward
|
0 comments:
Post a Comment