Thursday, September 12, 2013

MKUTANO WA CCM KITAIFA KUFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA CDT MJINI KAHAMA

 Katibu mkuu ABUDRAH KINANA akiwahutubia wananchi wa Kahama kwenye viwanja vya CDT Wilayani humo
 KATIBU mwenezi CCM Taifa NAPE NAUYE akiwahutubia wanchi  katika viwanja hivyo huku akiwataka wananchi hao kupuuza  upotoshaji unaofanywa na CHADEMA katika sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bungeni
 MWENYEKITI  wa ccm Mkoa wa Shinyanga  KHAMIS MGEJA alipokuwa akiwakaribisha viongozi  kitaifa katika mji wa Kahama mkoani humo


 KINANA akitoa mazito katika viwanja  hivyo vya CDT mjini Kahama
 KINANA akimurikwa  na vyombo mbalimbili vya habari  katika  hotuba zake alizotoa  katika ziara yake wilayani Kahama
 MBUNGE wa msalala {CCM} EZEKIEL MAIGE  akimweleza KINANA kazi iliyofanywa na ccm katika jimbo lake kuwa nipamoja  na  mradi wa maji  unaoendelea  jimboni kwake  ambapo umeanza kuwanufaisha wananchi wake
  MAIGE  akiendelea kuwakumbusha viongozi hao wa Kitaifa  uwjibikaji  wa chama Tawala
 KINANA akiendelea kuwa hutubia  wananchi waliojikusanya kumsikiliza
 KINANA akimkaribisha mbunge  wa viti maalumu wa  Shinyanga vijijini
 MMENYEKITI wa kitongoji  cha majengo NOELI MKURA  marufu kama MSEVEN  ambae pia ni kamanda wa kata ya majengo  akisimamia kikamilifu mstari watu wanaotaka kusogea  kwenye jukwaala la kuhutubia  viongozi
 KIONGOZI  huyo akiwa hutubia  wanchi wake kaitika viwanja hivyo
 BAADHI ya wananchi  waliohudhulia mkutano huo wakisikiliza kwa makini  hotuba ya viongozi wao
 KINANA  akitoa ufafanuzi  juu ya  ziara nzima kuhusu mchakato wa rasim ya katiba mpya  ilivyochangiwa na wananchi wa tanzania abapo amesema kuwa katiba haibadilishi maisha ya watanzania
 KINANA akiendelea kutoa hotuba zake katika viwanja vya CDT
 KINANA akiendelea kupokea kadi za CHADEMA zilizorudishwa na wanachama wa CHADEMA walio rejea kwenye chama  cha mapinduzi {CCM} wilayani Kahama
 MMOJA wa wanachama wa chadema ambao wamerudisha kadi; SHABAN SAID LUMELEZI  {28 }amesema kuwa hana sababu yakuendelea kuwa na CHADEMA kutokana hali aliyoiona  kwamba amegundua kuwa  CHADEMA ni kambale wenye masharubu na ndevu hivyo kwa hali hiyo yeye hawezi kukimbizana nao nakwamba yeye hana masharubu wala ndevu ameamua kurudi  kwa CCM ambayo haina sharubu wala ndevu  atawezana nayo
WANANCHI waangusha jukwaa kwa kugombaia kadi za CCM katika viwanja vya CDT mjini Kahama kutokana na ugawaji wa kadi hizo holela
 WANANCHI wakiwa katika viwanja vya CDT mara baada ya kuisha kwa mkutano
 BAADHI ya wana nzengo kutoka viji vya  Kahama wakigawana kadi za CCM




ENEO la nje ya soko la Nyihogo  latifuliwa  kwa kigezo cha kutengenezwa miundo mbinu mizuri  ya kiwango cha changarawe  lakini tangu matengenezo yaanze linaonekana kusahaulika hali inayowafanya wafanyabiashara wa  eneo hilo  kuona kuwa wameliwa kekundu na kusababisha bidhaa zinazopangwa nje ya soko hilo kujaa vumbi

HAWA NI VIJANA 2  MTU NA MDOGO WAKE ESTHER  na  CHEYO


Na Paul Kayanda,
Kahama,
Septemba 11,2013.

MKUTANO WA KINANA  WAPWAYA  KAHAMA.

MKUTANO wa Katibu Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi “CCM”wilayani Kahama uliofanyika juzi mjini Kahama ulipwaya
baada ya kukosa watu  wengi licha chama
hicho wilaya kutumia jitihada za kusomba wananchi kutoka kwenye Kata zote 54
kwa lengo la kuongeza mahudhurio.

Pamoja na matangazo mengi
kwenye magari mbalimbali yaliyokuwa yakipita mitaani ikiwemo kutangaza kupitia
redio moja mjini Kahama siku mbili kabla ya ujio wa kiongozi huyo wa
Kitaifa,lakini malengo ya kukusanya watu wengi hayakutimia.

Aidha katika viwanja hivyo
alipofanyia mkutano huo Katibu huyo wa CCM Taifa;Abdurhamani Kinana
aliyeambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM;Nape Nauye,pamoja na
Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Shinyanga;Khamis Mgeja lakini haukujaza kama
ilivyo kwa wanasiasa wengine.

Katika uwanja huo huo wana
siasa wengine wa vyama vya siasa,wakiwemo wabunge wamekuwa wakijaza watu wengi
pamoja na kutosomba wajumbe kutoka kwenye Kata hizo 54 zinazounda wilaya ya Kahama.

Pamoja na watu wachache
waliojitokeza wakiwa wengi ni viongozi wa CCM,Kinana alionekana kwenye hotuba
zake akilalamikia ufisadi wa Ardhi unaofanywa na watendaji wa serikali yake
hasa katika maeneo ya Halmashauri za wilaya,miji,manispaa na majiji.

Kinana alisema wananchi
wengi wamekuwa wakiporwa ardhi zao bila fidia hali ambayo wananchi inawafanya
waonyeshe kuichukia serikali yao ingawa baadhi ya wananchi wamedai udhaifu wa
viongozi wa chama hicho ngazi za juu ndio sababu inayochangia kuwepo kwa
ufisadi huo.

Akizungumzia mabadiriko ya
rasimu ya katiba mpya Kinana alisema idadi kubwa ya Watanzania wanataka
serikali tatu ambazo haziwezi kuwasaidia kwa kuwa zitakuwa na gharama kubwa ya
uendeshaji ambapo msimamo wa CCM ni serikali mbili.

Alisema serikali tatu
zitakuwa na majeshi matatu hali ambayo Rais wa Muungano akitangaza hali ya
hatari,Rais wa Tanganyika ama Zanzibar anakataa tayari hali hiyo itachangia kuibuka
kwa vita baina ya serikali hizo na kuvuruga umoja wa kitaifa.

Hata hivyo Kinana alisema
ataheshimu maamuzi ya wananchi wengi juu ya mabadiriko hayo watakavyoamua
pamoja na chama chake kuwa na msimamo wa Serikali mbili,ingawa hata baadhi ya
wana CCM wanapinga msimamo huo na kutaka Serikali tatu.

Katibu huyo yupo ziarani
Kanda ya Ziwa kuona utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi,ambapo wilayani
Kahama alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa .

MWISHO.
My Blogger Tricks
blogger

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KAYANDA All Right Reserved
Designed by MALUNDE.