HUHESO YAKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA HISABATI
Mshindi wa kwanza Doricas James Limbati,akipongezwa na Mwalimu wake Mkuu Lucas Matanyanga,mwenye T'Shirt ni Mkurugenzi wa Huheso;Juma Mwesigwa.Umati wa wazazi katika shule ya msingi Kahama ukishuhudia utoaji wa zawadi
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Kahama;Kapteni Mstaafu Robart Mabala akimpongeza mshindi wa tano;Martha Sungulwa.
WAZAZI
wametakiwa kuwa chachu ya kufanya vyema kielimu kwa watoto wao kwa kutumia
wasaa japo wa dakika tano kila siku kuketi
nao,kupitia madaftari ya masomo ili
kubaini udhaifu wao kisha kuwazungumzia umuhimu wa elimu jambo litakalosaidia
kuwajengea hamasa ya kufanya vyema katika mithani yao.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Shule ya Kahama;Kapteni mstaafu Robart Mabala,amesema hayo katika
hafla fupi ya utoaji zawadi kwa washindi wa somo la hisabati kwa wasichana
katika shindano lililoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la HUHESO
FOUNDATION lenye makao makuu yake Kata ya Malunga wilayani Kahama.
Kapteni
Mabala ametoa ushauri kwa wakazi wa wilaya ya Kahama mbali na kuketi na
kuwaelimisha watoto wao umuhimu wa elimu pia watumie fursa ya kuanzisha mfumo
wa mashindano katika suala la elimu jambo litakalosaidia kuleta maendeleo ya masomo kwa wanafunzi na kufanikiwa kuwapata
wasomi kama ilivyowahi kuwapata akina Jaji Ihema na wasomi wengine.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa HUHESO FOUNDATION;Juma Mwesigwa,amesema shirika lake
ambalo hujihusisha na masuala ya kijamii hususani katika masuala ya kuendeleza
kielimu watoto,liliona umuhimu wa kuanzisha shindano hilo lililohusisha watoto
wa kike ili kuwapatia hamasa ya kupenda som la hesabu.
Katika
shindano hilo lililoshirikisha wanafunzi wa kike 63 kutoka shule 15 za
Halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo awali lilitarajiwa kushirikisha wanafunzi
100 katika shule 20,huku zawadi ya mshindi wa kwanza ambayo ni Shilingi Laki
Moja ilichukuliwa na Doricas James Limbati kutoka shule ya msingi Nyahanga B.
Zawadi
ya Mshindi wa pili ilichukuliwa na wanafunzi watatu ambao ni Cecilia Kishiwa
kutoka Shule ya Msingi Busoka,Tatu Chatta kutoka Kahama B na Agness Boniphace
kutoka Majengo ambao walipata kila mmoja Shilingi Elfu Hamsini na zawadi ya
mshindi wa tatu ikienda kwa Martha Sungulwa wa Kahama B,ambapo zawadi ya
mshindi wa jumla ilichukuliwa na Shule ya Msingi Majengo iliyopatiwa mpira
mmoja wenye thamani ya shilingi Elfu Themanini.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment